Je, Luis Enrique yupo sahihi?

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Kocha wa timu ya Taifa ya Spain, Jose Luis Enrique ameita kikosi cha timu ya taifa kwaajili ya maandalizi ya Michuano ya Ulaya kwa Timu za Taifa zitakzoanza Juni 11 mwaka huu.

katika hali ya kushangaza hakuna mchezaji hata mmoja kutoka kwa wababe Real Madrid aliyeitwa kikosini humo.

Je, Luis Enrique yuko sahihi? Ataweza kuwapa Spain mafanikio kwenye Euro 2020 mwaka huu bila mchezaji wa Madrid?

 
Rekebisha mkuu apo bila spain, iwe madrid
 
Wapo wachezani wazuri tu Madrid, labda kama anaenda kamikisha ratiba tu
 
Real Madrid wamekuwa wachovu sana msimu huu, hawastahili kuwepo hapo.
 
Sidhani kama amefanya makusudi ila ni kutokana na hali kadha wa kadha za wachezaji wa Spain wanaochezea club ya Real Madrid.
Kwa mfano, Waliokuwa wakiitwa mara kwa mara ni pamoja na Sergio Ramos, Daniel Carvajal, Marcos Asensio, Lucas Vasquez na Isco.

Daniel Carvajal na Lucas Vasquez ni majeruhi, Sergio Ramos ametoka kwenye majeraha pia. Na bado anaendelea na hatua za kujiimarisha.

Marcos Asensio yeye ataenda Olympic japokuwa na yeye hakuwa na msimu mzuri, Isco na yeye amepotea mazima, labda mchezaji aliyestahili kuwepo kwenye kikosi ni Nacho Hernandez, kidogo msimu huu amekuwa katika kiwango kizuri.
 
Hata hivyo sidhani kama kuna mchezaji wa Madrid mhispania anayeweza kuitwa timu ya taifa, hii ni kutokana na majeraha, majukumu ya sehemu zingine na kiwango kidogo.
 
Siku wakiingia uwanjani wakakutana na ronaldo, bruno Fernandes, Ruben dias, Bernardo Silva na andrea silva ndio huyo kocha atajua kama alifanya makosa mpira sometimes unahitaji wazoefu kama Sergio Ramos.

Sent from my SM-J701F using JamiiForums mobile app
 
Ujerumani waliichukua Euro bila mastaa wake, waliichukua vijana tu Ndio wakabeba na ubingwa. Nadhani ukiondoa siasa za mpira ikibidi tuangalie ni mchezaji gani ameitwa ambaye Hafai, ambaye tungeweza kumtoa tukamuingia mchezaji wa real madrid. Mi mpaka sasa sijakiona kikosi labda aliyekiona aweke hapa
 
Kocha yupo sahihi ni yeye ndo anaamua nani amtumie kwenye timu yake
 

Euro ya mwaka gani hiyo?
 

Luis Enrique angekuwa black angekuwa na sura ngumu balaa
 
Kumuacha Ramos na Carvajal ni maamuzi sahihi, Ila Vasquez , Nacho na Assencio walistahiki kuwemo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…