Je, maadhimisho ya siku ya wakulima, maarufu kama nanenane yana tija yoyote kwa wananchi wa Tanzania?

Je, maadhimisho ya siku ya wakulima, maarufu kama nanenane yana tija yoyote kwa wananchi wa Tanzania?

Joined
Mar 15, 2018
Posts
26
Reaction score
36
"Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, ametangaza rasmi kurejea kwa Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi maarufu kama Nane Nane kwa mwaka 2022.

Waziri Bashe amesema baada ya timu ya Wizara kupitia na kubuni namna bora kulingana na mazingira ya sasa ya namna bora ya kuendesha maonesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mambo kadhaa yamefanyiwa maboresho na kushauri namna bora ya kuendesha maonesho hayo yenye zaidi ya miaka 27 tangu kuanzishwa kwake.

Waziri Bashe amesema jambo la kwanza ni kuyaendesha maonesho hayo ili kuwa endelevu; Kwa kuanzisha Vituo vya mafunzo kwa Wakulima msimu wote wa mwaka na wakati huo Vituo hivyo kuwa atamizi (Incubate) kwa Wakulima kwa kutumia teknolojia mbalimbali za kilimo kwa kipindi chote cha mwaka."

Jee kuna faida yoyote ambayo wananchi tunapata? kutokana na maadhimisho ya siku ya wakulima Tanzania ikumbukwe mwaka jana maadhimisho alihairishwa kwa tangazo la Waziri wa Kilimo wa wakati huo Prof. Adolf Mkenda; Tangazo alilitoa tarehe 10 Februari, 2021 Jijini Dodoma ambapo ilielezwa kuwa Serikali inafanya tathmini ya namna bora ya kuyaendesha maonesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) kwa namna bora.

1068px-Mt_Uluguru_and_Sisal_plantations-2.jpg
 
Kwa upande wangu yana faida kwa sababu napata kujifunza mbinu mbalimbali za kilimo, changamoto na hata mafanikio ya sekta ya kilimo Tanzania
 
Shida Watanzania( Wakulima) wengi ni wagumu kubadilika hata wafundishwe vipi ni 10% out of 100 ndo hubadilika. Aliekaribia kuibadilisha nchi hii ni Magu pekee
 
Yatakua na tija kama yaliyozungumzwa km masuala us punguzo la bei ya mbolea, mashamba Na mikopo kwa vijana pamoja Na vyuo vya mafunzo ktolewa katika hotuba Na kuwapo utekelezaji wa wazi wazi.

Pia ni sehemu bora ya wakulima kujifunza kuhusu kilimo, mazao ya kilimo na mnyororo wa thamani na kadhalika.
 
Weka Picha Mkuu ya Maonyesho ya Nane nane
 
Back
Top Bottom