Je, maandamano ya kuitisha kila mtu nchini bado ndiyo njia sahihi?

Je, maandamano ya kuitisha kila mtu nchini bado ndiyo njia sahihi?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
Kwa mtazamo wangu maandamano yanaweza kuwa na maana zaidi pale yanapokuwa na kundi maalum lenye madai yanayoeleweka na yanayohusu moja kwa moja maslahi yao kwa mfano wafanyakazi, wanafunzi, madereva au kundi fulani la kijamii.

Kwa mfano wanasiasa au wanaotaka kugombea nafasi kwenye uchaguzi wana ji organize wanaadamana na mabango yao mpaka labda viwanja fulani wakidai tume huru ya uchaguzi kwa inakuwa wachache na ujumbe wao unafika na hata policccm wanakuwa hawana sababu ya kuyazuia kwa sababu unakuta labda ni watu 1000 tu wameamua kuandamana na kwenda front wengine wanabaki wanashambulia mitandaoni namaanisha wafuasi sasa, Hapo mtu anaweza kuelewa kabisa: “Hawa watu wanataka nini, na kwa nini wamefika hapa?”

Lakini kuitisha kila mtu nchini bila kuweka madai yanayotekelezeka kwa uwazi kunaweza kufanya ujumbe upotee na hata kuwapa nafasi watu wenye nia nyingine kuingia kwenye kundi hilo.

Pia kuna tofauti kati ya kuonyesha hisia na kutegemea jambo libadilike mara moja. Kama madai fulani yanahitaji mchakato mrefu wa kisera au kisheria, ni muhimu kuwa na mkakati unaoeleweka badala ya kutegemea tu idadi kubwa ya watu barabarani.

Vinginevyo unaweza kukuta watu wamekusanyika wengi, lakini ukiwauliza “tumekuja kudai nini hasa?” majibu yanakuwa tofauti..
 
Kwa mtazamo wangu maandamano yanaweza kuwa na maana zaidi pale yanapokuwa na kundi maalum lenye madai yanayoeleweka na yanayohusu moja kwa moja maslahi yao kwa mfano wafanyakazi, wanafunzi, madereva au kundi fulani la kijamii.kwa mfano wanasiasa au wanaotaka kugombea nafasi kwenye uchaguzi wana ji organize wanaadamana na mabango yao mpaka labda viwanja fulani wakidai tume huru ya uchaguzi kwa inakuwa wachache na ujumbe wao unafika na hata policccm wanakuwa hawana sababu ya kuyazuia kwa sababu unakuta labda ni watu 1000 tu wameamua kuandamana na kwenda front wengine wanabaki wanashambulia mitandaoni namaanisha wafuasi sasa…Hapo mtu anaweza kuelewa kabisa: “Hawa watu wanataka nini, na kwa nini wamefika hapa?” Lakini kuitisha kila mtu nchini bila kuweka madai yanayotekelezeka kwa uwazi kunaweza kufanya ujumbe upotee na hata kuwapa nafasi watu wenye nia nyingine kuingia kwenye kundi hilo.


Pia kuna tofauti kati ya kuonyesha hisia na kutegemea jambo libadilike mara moja. Kama madai fulani yanahitaji mchakato mrefu wa kisera au kisheria, ni muhimu kuwa na mkakati unaoeleweka badala ya kutegemea tu idadi kubwa ya watu barabarani. Vinginevyo unaweza kukuta watu wamekusanyika wengi, lakini ukiwauliza “tumekuja kudai nini hasa?” majibu yanakuwa tofauti..
Tinachohitaji ni kuwasilisha ujumbe wetu hayo mengine kayajadilini kwenu lumumba
 
Back
Top Bottom