Je, madai ya Hellen White yana ukweli kuwa shetani na malaika zake walitubu dhambi baada ya uasi lakini Mungu aligoma kuwasamehe?

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Wadau hamjamboni nyote?

Naomba kujua kama upo ushahidi wa Maandiko kuthibitisha madai kuwa Shetani na Malaika zake baada ya uasi mbinguni waliamua kumlilia Mungu wao awasamehe ila aligoma?

Nimeweka nukuu ya Mama Hellen G White Nabii wa Wasabato hapo chini.

"After Satan was shut out of heaven, with those who fell with him, he realized that he lost all the purity and glory of heaven forever. Then he repented and wished to be reinstated in heaven. He was willing to take his proper place, or any place that might be assigned him.

He and his follower repented, wept and implored to be taken back into the favor of God. But no, their sin their hate, their envy and jealousy, had been so great that God could not blot it out. It must remain to receive its final punishment"

Nukuu hiyo imetoka kwa kitabu cha (Spiritual Gifts, vol. 1, p. 18, 19).

Karibuni tujadili kwa hekima kubwa na kwa mifano halisi

Usiku mwema wapendwa
 
Hakuna Malaika walioomba Msamaha.

Yuda 1:6

Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
 
Nini lengo lako?kujifunza au ligi au una agenda yako nyuma ya pazia?
 
Ili kuziamini dini inabidi uwe fala fala fulani,ujitoe akili na usiumize akili kuwaza sana mana dini ni upuuzi uliojaa soga.
 
Fiction stories hizo na ma fiction characters yasiyo kuwepo ndio maana yana utata.

Shetani, Mungu, pepo, jehanamu, kuzimu ni Hadithi za kusadikika na kufikirika.

Imagination just an illusion.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Una miaka mingapi mkuu?
 
Makanisani tunafundishwa kuwa mwenyezi Mungu ni mwenye huruma sana na umsamehe mwenye dhambi yeyote anaeomba msamaha kwake hata kama dhambi zake ni nyekundu kupitiliza. Je, huruma na msamaha wa aina hiyo unawahusu binadamu tu na wala hauwahusu viumbe wake wengine kama huyo shetani na malaika walioasi na baadae kuomba msamaha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…