Je madaraja ya Bima za Magari yanaweza kubadilishwa?

grafani11

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2011
Posts
15,441
Reaction score
5,816
Kwa wale wataalamu wa masuala ya Bima za magari nawaomba mnijuze.

Jamaa yangu amenunua gari mkononi mwa mtu, gari yenyewe imelipiwa bima premium ambayo inatarajiwa kuisha mwishoni mwa mwaka huu. Yeye hataki kulipia bima hiyo "premium" anataka "third party", alinifuata kuomba ushauri kama anaweza kubadili na kulipia "third party".

Kwa kuwa mimi sio mtaalamu wa mambo haya nikaona nililete hili kwenu waheshimiwa ili mumshauri ipasavyo. Gari yenyewe ni Toyota Carina TI.
Karibuni.
 

Mkuu this is simple inawezekana kabisa...mteja ndio anaamua ni bima gani anataka alipe na anainsure kiasi gani. hjawawezi kumlazimisha aendelee na comprehensive kama mwenyewe hataki/hana uwezo.....japo comprehensive ni nzuri na ndio inabeba maana hasa ya Bima

CC charminglady
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,

Hili neno "PREMIUM" unalitumia ndivyo sivyo.
Premium maana yake ni MAKATO.

Kwa usahihi labda ulimaanisha COMPREHENSIVE. Na kama ndio basi hiyo inawezekana tu.
 
Mkuu,

Hili neno "PREMIUM" unalitumia ndivyo sivyo.
Premium maana yake ni MAKATO.

Kwa usahihi labda ulimaanisha COMPREHENSIVE. Na kama ndio basi hiyo inawezekana tu.
Ahsante mkuu, ndiyo hiyo hiyo. Siunajua tena sisi wengine hatuna utaalamu zaidi, tunajua kulipa tu kuepuka usumbufu barabarani hasa baada ya kupata simu ya Agent kukumbushia kulipia basi. Hata na kuisoma cover note hatukuwa na muda.
 
Heshima kwako mkuu Kaizer, nashukuru kwa taarifa.
 

Ndio Inawezekana kabisa.... Katika BIMA kuna notification flani hivi naona watu wengi huwa hawaitilii maanani make pia imandikwa kwa herufi ndogo labda ndio sababu. Na watu wengi huwa hawasomi "policy" zao ama covernote "hati ya Bima" maneno hayo yanasomeka hivi:-

"In the event of any change of ownership or change of vehicle, this certificate "hati ya bima" becames invalid and must be returned toe the Company within seven days of the change"

Kwa maana hiyo unaponunua gari, ile bima iliyopo kwenye lile gari inakuwa INVALID kwa sababu imeandikwa kwa jina la yule aliyekuuzia. Unaponunua gari ambalo limekwishakatiwa BIMA na ukabadilisha jina na kutumia jina lako, nenda kalipie bima upya. Ile bima ya yule mtu sio yako, ila wabongo tulivyo mabandidu mpaka ile bima iishe ndipo tunakata nyingine!
 
lakini insurance ni biashara inayotajirisha watu fulani wachache na kunyonya wengi
 
Dada Charminglady ni kweli hata mimi hiyo sehemu sijaipitia, cover note zangu ninazo lakini najua kulipia tu sisomi.

Nashukuru sana kwa elimu ya kutosha.
 
Hii nina uhakika si watu wote wanaifahamu, kwa sababu nimeshakuwa shahidi wa watu wengi kwenye ununuzi wa Magari. Swali lao la kwanza kabla ya kununua gari wanauliza kama vibali vyote vipo valid (Bima na Road licence), bahati mbaya wengi hawaoni umuhimu wa ku-change ownership kwa sababu hawasumbuliwi na vyombo vya dola barabarani.
 
lakini insurance ni biashara inayotajirisha watu fulani wachache na kunyonya wengi

Huwezi kuiona faida yake mpaka utakapokutana na majanga. Thats why its called insurance aka bima kwa lugha za kindengereko (kinga dhidi ya majanga)
Hatukati bima baada ya janga. Tunakata bima kabla ya janga ili in case janga hilo litatokea then we are well covered.
The good thing about this life, we always live happily kwa sababu hatujui kesho kuna nini au hapo mbele kuna nini.
Nafikiri utakuwa umenielewa walau kiduchu
 
nimekuelewa kaka lakini sasa kama sijapata janga wasichukue mshiko wote angalau iwepo asilimia fulani inayorudi kwa anayelipa, sasa wao wanachukua kila kitu bana........
 
nimekuelewa kaka lakini sasa kama sijapata janga wasichukue mshiko wote angalau iwepo asilimia fulani inayorudi kwa anayelipa, sasa wao wanachukua kila kitu bana........

Ndo biashara ya bima ilivyo mkuu. Ukinunua bima wao wanajicommit kukulinda kipindi cha majanga yako na kukurudisha mahala pa mwanzo ulipokua baada ya janga.
Ni sawa na kwenda dukani na kutaka kununua TV then uende nayo kwako kuitumia ila hutaki kulipia hela yote.
Haiwezekani.
 
kitu kingine ambacho hawa jamaa wa insurance inabidi wajirekebishe ni usumbufu baada ya mteja kupata matatizo....ninafahamu watu waliosumbuliwa sana kwenye kulipwa
 
kitu kingine ambacho hawa jamaa wa insurance inabidi wajirekebishe ni usumbufu baada ya mteja kupata matatizo....ninafahamu watu waliosumbuliwa sana kwenye kulipwa

Usumbufu utategemea sana na jinsi ulivyokamilisha documents zako mkuu.
Ukiripoti ajali mapema katika mamlaka stahili, ukakamilisha nyaraka zote zinazohitajika sidhani kama itakuchukua mda sana kulipwa madai yako. Ukiona unacheleweshwa basi ujue lazima kuna walakini kwenye makabrasha yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…