Je, Mahabusu zetu zina vyumba maalum (VIP) kwa watu maarufu kwa usalama wao?

Kuna picha zilitolewa zikiwaonyesha Basil Mramba na Daniel Yona wakiwa mahabusu ya gereza yaaani ni special treatment maana ile selo ilikuwa imekarabatiwa safi na imepigwa nakshi nakshi halafu waliwekewa kiti kwenye difenda ahahahah
 
Kuna mahabusu za polisi hizi hazina VIP.

Magereza Kama Keko wana sell za VIP.

Utofauti ni kwamba wanalala wachache na magodoro safi.

Kuhusu nani akae VIP hiyo inategemea maamuzi ya bwana jela haitegemei umaarufu wako.

Wapo wanaowekwa VIP kutokana na usalama wao either ni mtuhumiwa ambaye anao wenzake na yeye anaonekana ni shahidi mzuri wa kesi.

Pia wapo wanao toa mlungula ilo wakae huko.

Kuhusu chakula, chakula kipo kwa mahabusu wote. Kuna magereza hawaruhusu chakula kutoka nje lakini kama Keko uwe kajambanani au VIP unaweza kuletewa chakula kutoka nje Kama nduguzo wana huo uwezo.

Kuhusu kuchanganywa na wafungwa, mfano Keko na Segerea ni magereza ya mahabusu wafungwa waliopo ni wafanyakazi ambao hushiriki kufanya usafi wa nje na maofisi na pia kupika, unaweza kuchanganywa na wafungwa mchana ila kulala mahabusu peke yao na wafungwa peke yao.

Mavazi unavaa yako kutoka nyumbani na ukihukumiwa orange inakuhusu.

Matibabu Kila gereza lina daktari na siku ukiingia unatakiwa kudeclare matatizo ya kiafya uliyonayo Kama bwana jela atahitaji kujiridhisha utatakiw kutoa vithibitisho. Mahabusu hupelekwa hospital akizidiwa au akiwa na ugonjwa ambao unahitaji daktari wa nje.

Keko Kuna selo ya wagonjwa ambao wanahitaji huduma Kila wakati.

Kukaa VIP inategemeana unaweza ukawa unataka au hutaki. Kwa Sabaya mfano kwa cheo chake anaweza akapewa VIP lakini kwa kesi aliyonayi hilo litamzuia kuwasiliana na wenzake, kwenye kesi mipango.
 
Mimi pia nahisi kitu Kama hiki
 
Mimi pia nahisi kitu Kama hiki
 
Huko mahabusu ukipelekwa unatakiwa umenyeke kweli kweli
 
Mkuu asante kwa majibu yako mazuri
 
Sabaya anatakiwa akapelekwe mahabusu ambayo ndani kuna wale aliowaweka yeye mahabusu kwa kesi za kusingiziwa ili wamgeuze mke, aliwe jicho apate mimba
 
Sabaya anatakiwa akapelekwe mahabusu ambayo ndani kuna wale aliowaweka yeye mahabusu kwa kesi za kusingiziwa ili wamgeuze mke, aliwe jicho apate mimba
Kuna mdau kafunguka hapo juu. Kama una maadui humo ndani itabidi upewe VIP.
 
Stori za Vijiweni: Miaka fulani palikuwa na mahakama ya kimataifa iliyokaribishwa kufanyikia TZ. Watuhumiwa walipohukumiwa, TZ ilipewa ofa ya kuwafunga waliokutwa na hatia. TZ ilipoteza fursa ile kwa vile hakukuwa na gereza linakidhi vigezo vya kimataifa kumfunga binadamu.

Nchi nyingine za Kiafrika zilikuwa zishachangamkia fursa. Zikawa zinakula pesa za kigeni kwenye magereza yao waliyoyajenga mahsusi.

Pengine ipo haja sasa ya kujenga (ma)gereza kwa viwango vya kimataifa.
 
Kwanini wasijenge na Aridhi ya kutosha ipo?
 
Hadi simu alikuwa anapiga kama kawaida mpaka magu akamuhamisha mkuu wa gereza πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…