Je, majasusi kutoka ughaibuni wanatumia NGOs za Afya kuja kupeleleza nchi za kiafrika?

Je, majasusi kutoka ughaibuni wanatumia NGOs za Afya kuja kupeleleza nchi za kiafrika?

Tuusahau ushetani wa CCM kidogo katika suala hili...

Habari za kuweka idadi ya viwanda imekushinda, saa hii unachomekea vijihadithi vya kipumbavu ili kuvuta muda. Tanzania ina kipi cha kufuatiliwa na wazungu?
 
Habari za kuweka idadi ya viwanda imekushinda, saa hii unachomekea vijihadithi vya kipumbavu ili kuvuta muda. Tanzania ina kipi cha kufuatiliwa na wazungu?
Mjomba kuna thread ya utekelezaji wa ilani ya CCM nitaileta...hapo utapata habari ya viwanda ...usidilute mada
 
Tuatokaje huko sasa..kama hatutafakari haya kwa kina??

Kama maana yako ni hii nafikiri ni vyema ukaanzisha mjadala mwingine, kwa mjadala huu ukisoma comment za wengi utapata majibu kuwa Wazungu kutuchunguza sisi au kututawala sio kazi ngumu kwao na pia mpaka sasa hatuna uwezo wa kubishana nao maana tayari tunawategemea kwa zaidi ya 90% kuliko wanavyotutegemea sisi..

Anzisha mjadala mwingine kwa maana kama unamaanisha " tufanyeje tujikwamue na kujitegemea?"
 
Wale jamaa wakihitaji kujua hadi ya jikoni...
Walimdukua kiongozi wa Taifa kubwa linaloongoza Ulaya. Teknolojia ndio uchawi Mkuu kwao hapo ndio wametuweza sana.
 
Acha mada za kijinga, hakuna chochote cha kusumbua wazungu hapa Tanzania.
Sisumbui wazungu mkuu...naleta hoja ya kutafakari kama vijana wa Taifa hili
 
Haya ni mambo fikirishi kutokana na experience yangu ya kuona mambo mbalimbali.
Je kama watanzania tumejiandaa vipi kukabiliana na uwezekano wa hali hii?

Ieleweke kuwa Afya ni eneo nyeti katika mustakabali wa nchi na wananchi.
Aidha ni muhimu kujua kuwa vita baridi vinaweza kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo mipango mikakati na ya muda mrefu katika kudhoofisha afya au kuhadaa umma hivyo afya ni tool muhimu ya vita.

Nisiwachoshe sana bali ni muhimu kama jamii tufikiri kwa kina aina za vita au hujuma zinazoweza kutumika kupitia sekta ya afya.

Umakini mkubwa unahitajika katika usimamizi wa Sekta hii.

NGOs nyingi nchini zinaingia kwa gear hii je zinafuatiliwa kwa jicho la afya na jicho la usalama??

TUTAFAKARI!MWENYE KUELEWA ANANIELEWA !

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!

Kwa teknolojia waliyo nayo hao mabeberu, sidhani kama wanahitaji kuleta mtu yoyote kuja kutuchunguza maana taarifa zetu zote wanazo huko huko waliko. Kila tunachofanya huku wana uwezo wa kukiona wakiwa huko huko bila tatizo lolote. Na hata wakiamua kutuangamiza sidhani kama kuna mwenye la kufanya.
Hata hivyo uwezekano wa kutuangamiza ni mdogo kwavile pia sisi ni soko lao kubwa, sanasana watuongezee magonjwa ili tuendelee kutumia rasilimali zetu kununulia madawa kutoka kwao na kuendelea kuwatajirisha.
 
Jingalao

ARV unapewa bure.
Condom unapewa bure.
Zaidi ya 50% ya budget wanakupa wao.
Zaidi ya 50% ya viongozi wako wamesoma kwao.
Gari unalotembelea wametengeneza wao.
100% ya zana za kijeshi wametengeneza wao na nyingine wamekupa msaada.
Madini unayochimba wao ndio wanunuzi.
Dini mnazoabudu wao ndio walileta.
Internet mnayotumia ni wao wagunduzi.
Laptop zenu zote mnazotumia ni wao.
Simu za mkononi hizo iphone ni zao..
OS kwenye mifumo yenu ni zao..
Wao wana drones huna uwezo wa kuziona.
Kule angani wameweka satelite na wanaona kila kitu..

Mimi nafikiri tuendelee tu kula ugali tuache kelele..

Kwakweli hapa tulipo tumeshikwa pabaya na ni ngumu mno kujinasua kwenye huu mtego.

Sisi tuendelee kula ugali mkuu.
 
NGO zote hasa zile kubwa na zenye mafungamano na taasisi kubwa za nje ya nchi hususan Ulaya na Marekani ni majasusi tu
 
Waje kuwapeleleza mara ya Pili kama waliweza tumia wamissionary kuja kuwapeleleza na hatimae kuwawatala na kuwauza kama watumwa karne kama 4 na baadae wakawapa uhuru wa bendere na kendelea kuwatawala Indirect waje kuwapeleleza tena mkiwa na jipya gan kuwajengea vyoo.???? Mzungu anawajueni nje ndani hamna jipya la kumtisha hasa nyinyi ngozi nyeusi


Blackberry
 
nimeona Mengi mkuu...nimepata uzoefu wa mengi mkuu
Huo sio mzizi wa tatizo, halafu ingependeza kama unge share mambo mawili matatu hivi ili kuupa mashiko huu uzi. Uko too general..content ipo ila hakuna details za ku trail au ku reflect na contents.

Kwa sababu umeruka kitu kimoja cha msingi. Elimu! Huko ndio wanatupiga kuanzia kutuwekea mitaala ya kurahisisha yao..na kututoa nje ya mazingira yetu. Ambapo elimu ingekuwa bora hata hiyo misaada ya afya na chanjo ingefanyika home hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo sio mzizi wa tatizo, halafu ingependeza kama unge share mambo mawili matatu hivi ili kuupa mashiko huu uzi. Uko too general..content ipo ila hakuna details za ku trail au ku reflect na contents.

Kwa sababu umeruka kitu kimoja cha msingi. Elimu! Huko ndio wanatupiga kuanzia kutuwekea mitaala ya kurahisisha yao..na kututoa nje ya mazingira yetu. Ambapo elimu ingekuwa bora hata hiyo misaada ya afya na chanjo ingefanyika home hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Great thinker endelea kutafuta Ukweli utaupata
 
Mheshimiwa Magufuli ametupa nguvu kubwa kupambana na wafadhili wasanii
 
Sasa hao majasusi kwenye nchi maskini kama hii wanachunguza nini?
Mimba za utotoni?
Mauaji ya albino?
Uchawi wa Gamboshi?
ACHENI MAJUNGU HAO WENZETU WAPO MBALI TAYARI LAZIMA TUSHIRIKIANE NAO, HATA HUYO BOSI WENU ANAEWAOGOPA HAO WAZUNGU SIKU AKIUMWA TU MNAMKIMBIZA WAKAMTIBU.

NYERERE, MUGABE NA VIBULI VYAO VYOOTE WALIFIA KWENYE HOSPITALI ZA WAZUNGU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom