Je, maji ya bahari yana matumizi gani?

Hammy Js

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2017
Posts
3,054
Reaction score
3,263
Jana mida ya jioni nilikua pale Kivukoni ferry nikimsubiri mtu, ghafla akaja mdada wa makamo anaelekea kwenye utuuzima hivi.

Yule mdada alikuja na gari yake ndogo hivi, akashuka kwenye gari huku akiwa na kidumu chake mkononi.

Alivuka ule ukingo ambapo mara nyingi watu wanakaaga na kuingia kwenye maji (ilimchukua muda sana mana alikua anaona aibu). Mwisho akaamua liwalo liwe, akajitosa na kidumu chake na kuanza kuchota yale maji.

Alipomaliza kuchota,akachukua mfuko wake wa rambo kwenye sketi yake na kuingiza kidumu chake. Watu wote tulikua tukimshangaa kuanzia pale alipokua anaanza kuvuka ule ukingo,kuchota maji na hata wakati anaondoka watu bado tulikua tukimshangaa.

Nilimuuza jirani yangu kuhusu matumizi ya yale maji maana kwa harufu ya yale maji,sidhani kama yanafaa hata kuogea lakini naye hakuwa na jibu.

Je maji ya bahari ya bahari yana matumizi gani?
 
Hujawahi kusikia kauli hii:

"Nitaogea maji ya bahari kuondoa hii gundu".

"Kaoge maji bahari"

Huyo dada alikuwa na mikosi yake na hapo alienda kujitakasa.
 
Hujawahi kusikia watu wakiambiwa kuwa wana kimavi hivyo wanapaswa kuogea maji bahari?
 
Hujawahi kusikia kauli hii:

"Nitaogea maji ya bahari kuondoa hii gundu".

"Kaoge maji bahari"

Huyo dada alikuwa na mikosi yake na hapo alienda kujitakasa.
Duh kaaazi kweli kweli,kwahyo mtu akiogea mikosi inaondoka kweli?
 
Unajuwa wewe unashangaza ina maana huko ufukweni ulipokwenda hujaona watu wakiogelea baharini? Mpaka useme maji ya bahari hayafai kuoga?
 
Unajuwa wewe unashangaza ina maana huko ufukweni ulipokwenda hujaona watu wakiogelea baharini? Mpaka useme maji ya bahari hayafai kuoga?
Harufu ya maji ya ferry unaijua vizuri?
 
ushetani tu...
Ushetani kivipi?

Tulipokuwa wadogo enzi hizo tulikuwa tukipanda Icarus kwenda Posta kwa ajili ya kuchota mchanga wa bahari tu na kuja kukaangia karanga ndio zilikuwa biashara zetu ndogo ndogo za kutusaidia vijisenti vya kujikimu shuleni.
 
Harufu ya maji ya ferry unaijua vizuri?
Hakuna maji ya ferry, kuna maji ya bahari.
Harufu unayoisikia wewe ni bahari inapumuwa ina maeneo maalum na muda maalum ya kupumulia hata ocean road, Sealander bridge na Coco beach.
 
Hakuna maji ya ferry, kuna maji ya bahari.
Harufu unayoisikia wewe ni bahari inapumuwa ina maeneo maalum ya kupumulia hata Sealander bridge na Coco beach.
Kaoge mkuu halafu panda daladala kama hujaachwa usafiri peke yako
 
Ukishakuwa huna imani na Mungu katika maisha yako kila utakachoambiwa unaweza kujikuta unafanya..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…