Jana mida ya jioni nilikua pale Kivukoni ferry nikimsubiri mtu, ghafla akaja mdada wa makamo anaelekea kwenye utuuzima hivi.
Yule mdada alikuja na gari yake ndogo hivi, akashuka kwenye gari huku akiwa na kidumu chake mkononi.
Alivuka ule ukingo ambapo mara nyingi watu wanakaaga na kuingia kwenye maji (ilimchukua muda sana mana alikua anaona aibu). Mwisho akaamua liwalo liwe, akajitosa na kidumu chake na kuanza kuchota yale maji.
Alipomaliza kuchota,akachukua mfuko wake wa rambo kwenye sketi yake na kuingiza kidumu chake. Watu wote tulikua tukimshangaa kuanzia pale alipokua anaanza kuvuka ule ukingo,kuchota maji na hata wakati anaondoka watu bado tulikua tukimshangaa.
Nilimuuza jirani yangu kuhusu matumizi ya yale maji maana kwa harufu ya yale maji,sidhani kama yanafaa hata kuogea lakini naye hakuwa na jibu.
Je maji ya bahari ya bahari yana matumizi gani?