inamankusweke
JF-Expert Member
- Apr 24, 2014
- 20,344
- 21,967
Airtel wezi,sinunui Tena mb,yaani GB 1 kusoma jamiiforums kwa siku inaisha!?..nazima data nikiwa na mb 150,kesho asubuhi meseji inakuja mb zimeisha wakati sijawasha dataNaomba anayefahamu atueleze, kuna kitu gani kinachoendelea katika hii mitandao ya simu kwa sababu inaonekana ni wizi wa dhahiri kabisa.
Kwa mfano, kwa sasa ukinunua GB moja ambayo ni sawa na MB 1,000 na kama hutumii kwa kupakua ila kwa ku-browse tu pale ambapo ulikuwa ukitumia kwa takriban siku 5 sasa utatumia kwa siku moja na nusu tu na sio zaidi ya hapo na huu mchezo umeanza kama siku mbili tu zilizopita..!!!!
Je haya makampuni hasa Airtel na Vodacom ambazo ndizo ninazitumia zaidi wanaweza wakatueleza kuna nini hapa kabla hatujafuatilia TCRA???? Maanake ni wazi kabisa kwamba huu ni wizi wa wazi kabisa.