Je, Makardinali ni raia wa Vatican?

Je, Makardinali ni raia wa Vatican?

09 July 2023

PAPA FRANCIS AMTEUA MONSIGNORE PROTASE RUGAMBWA AMBAYE NI ASKOFU WA JIMBO LA TABORA TANZANIA KUWA KARDINALI
1689024583141.png

Baba Mtakatifu Papa Francis akiwa dirishani St. Peter's Square alipo toa taarifa za uteuzi

Shughuli rasmi ya kumpa cheo hicho na makadinali wengine wateule itafanyika mwezi September tarehe 30, 2023 Papa Francis ametoa taarifa hiyo katika St. Peter's Square leo

Makadinali wengine wapya wateule wanatoka nchi za United States, Italy, Argentina, South Africa, Spain, Colombia, South Sudan, Hong Kong, Poland, Malaysia, Tanzania, and Portugal.

Makadinali - wateule huvishwa bereta ile kofia nyekundu ya ukadinali na kuvishwa pete yenye nembo maalum inayoashiria kuwa Prince of the Church kuwa nembo ya washauri wakuu wa Baba Mtakatifu ambaye ni kama King of the Church. Hivyo makadinali ni kama watoto wanaoendeleza kanisa na ni washauri wakuu wa Papa.

Kazi nyingine ya makadinali ni kushiriki katika conclave ya kumchagua Baba Mtakatifu yaani Papa inapotokea hitaji hilo la kuchaguliwa Papa kumrithi baba mtakatifu aliyekuwepo ndani ya kanisa. Kuna kanuni Kadinali akifikisha miaka 80 ya umri asiwe na haki ya kupiga kura kuingia katika conclave ya kumchagua Baba Mtakatifu. Hali ya kiafya ikiwa siyo nzuri ya kadinali hata kama hajafikisha umri wa miaka 80 haruhusiwi kushirikia conclave ya kumchagua Baba Mtakatifu yaani Papa.

Tanzania imepata heshima pia huko nyuma kuwa na Kardinali Polycarp Pengo mwaka 1998 baada ya kufariki kwa Kardinali Laurean Rugambwa mwaka 1997. Kardinali Laurean Rugambwa ambaye alikuwa mwaafrika wa kwanza kuwa cardinal mwaka 1960.


26 Juni 2023

Salamu za Rais Samia kwa Askofu Mkuu Mwandamizi Protase Rugambwa zikiwasilishwa na Waziri Nape


Mh. Samia Hassan anasema Baba Askofu Protase Rugambwa ni hazina na tunda jema la kiroho la Tanzania na Afrika kwa jumla

PICHA TOKA MAKTABA :
Papa akiwa na askofu Protase Rugambwa
1689024179623.png
 
Askofu jimbo kuu katoliki la Tabora kadinali-mteule Protase Rugambwa akielezea alivyopata taarifa ya uteuzi kwani nilikuwa katikati ya ibada ... mimi ni raia mtanzania kwanza halafu mengine yanafuata na heshima hii ni kwetu wote waTanzania wa ...

 
Kadinali mteule Askofu Protase Rugambwa nimezaliwa Bunena Bukoba, Tanzania kwetu ni Karagwe kiasili na jina hili la Rugambwa nimepewa kwa heshima ya tukio kubwa la mwaka 1960 ...

 
Sio kweli kuwa Makardinali wote ni mawaziri wa Vatican. Kwani hata His eminence Protase Cardinal elect Rugambwa alikua Waziri akisimamia wizara ya Uinjilishaji wa watu akiwa si kardinali. Hitaji la msingi kila Waziri wa Vatican lazma awe walau Askofu mkuu.
Ad majorem Dei gloriam.
 
Katiba ya Tanzania hairuhusu uraia wa nchi mbili, ila katikan hili Kanisa Katoliki lipo juu ya Katiba.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23],Nimecheka utadhani mazuri.Kanisa Katoliki halipo juu ya Katiba ya nchi yetu.Mpendwa km kitu hukijui bora uulize wataalamu wa Elimu ya Uraia wakufundishe kuliko kuhukumu Kanisa moja kwa moja.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23],Nimecheka utadhani mazuri.Kanisa Katoliki halipo juu ya Katiba ya nchi yetu.Mpendwa km kitu hukijui bora uulize wataalamu wa Elimu ya Uraia wakufundishe kuliko kuhukumu Kanisa moja kwa moja.
Hili la Holy Sea mbona lipo wazi sana!
 
Tukiwa bado tunasherehekea kuteuliwa Kwa Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa ambae ataapishwa huko Vatican tarehe 30 Septemba.

Ni vema kutambua Makardinali ndio humchagua Papa, kupitia haki hiyo ya kupiga kura ya kumpata Rais wa Vatican (Baba Mtakatifu) je, Makardinali Wana uraia wa Vatican?
Na ndio washauri wa Papa. Wanatengeneza kitu kinaitwa Curia. Ni watu muhimu katika kazi za Askofu wa Roma(Pope)

Ingawa hii chenga ya mwili imeniweka kwenye fikra kubwa sana. Tulizoea Cardinal lazima awe Dar. lakini Mwenyezi Mungu, kwa hekima yake ameamua sasa awe Tabora.
Kanisa katoliki katika ubora wake....
 
Katiba ya Tanzania hairuhusu uraia wa nchi mbili, ila katika hili Kanisa Katoliki lipo juu ya Katiba.
Mwadhama Polycarp akisafiri nje ya nchi hutumia passport ya Vatican ambayo ni Diplomatic! Kanisa Katoliki halibanwi na mamlaka ya nchi yoyote!
Kuna baadhi ya nchi kama Msumbiji kanisa haliruhusiwi kutangaza askofu bila kuishirikisha serikali na serikali ikikataa hatangazwi au atatangazwa kwa siri! Jambo hili huliuzi sana kanisa maana mamlaka yake yanakuwa sio absolute!

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Mwadhama Polycarp akisafiri nje ya nchi hutumia passport ya Vatican ambayo ni Diplomatic! Kanisa Katoliki halibanwi na mamlaka ya nchi yoyote!
Kuna baadhi ya nchi kama Msumbiji kanisa haliruhusiwi kutangaza askofu bila kuishirikisha serikali na serikali ikikataa hatangazwi au atatangazwa kwa siri! Jambo hili huliuzi sana kanisa maana mamlaka yake yanakuwa sio absolute!

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Hakuna sehemu yoyote ile serikali inachagua Askofu wa Roma. Nilisikia wali compromise China. Sababu ni kuwa, hawataki kubeba mtu wasiyemjua.
Kanisa limesheheni spies wa aina zote. Lina namna ya kujua nyendo na changamoto za watumishi wake wote. Ingawa kwa muda mrefu limekuwa linawastahi baadhi ya walioteteleka, kwa kuwalinda au kutowatoa nje wakapata hukumu za matendo yao.
 
Back
Top Bottom