Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,437
- 13,836
Wanasema mzaha mzaha hutumbua usaha, kwa mujibu wa katiba yetu, mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa ni jambo la muungano, hii ni pamoja na misaada pamoja na mikopo kutoka nje ya nchi. (Katiba ya JMT ibara ya 4 nyongeza ya kwanza)
Lakini tangu awamu ya sita ya rais wetu Samia Suluhu ishike hatamu, kumekuwa na jambo la kushangaza linaendelea Zanzibar, mabalozi wa nchi mbalimbali hususani za magharibi pamoja na wajumbe wa mashirika ya kimataifa wamekua wakifanya ziara Zanzibar pamoja na kukutana na kufanya vikao na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Mikutano hiyo imekua ikilenga kuongeza ushirikiano baina ya mataifa hayo na Zanzibar. Na baadhi yao wamemwaga ahadi za misaada kwa Zanzibar.
Je, mwenendo huu wa Zanzibar na mataifa hayo ya nje ni sawa? Nini hatima ya muungano wetu?