Je, mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa sio jambo la muungano? Nini kinaendelea Zanzibar?

Hao wengine ni wajinga wajinga tu, mradi wapayuke tu.
 
Wazanzibari wana-petition hadi UN kutaka mamlaka kamili ya nchi yao, sisi tunaona wanafanya yasiyoendana na tulivyokubaliana tunapiga miayo tu!

Take reciprocal action.
Lengo ni tuwe na serikali moja, tutafika tu.
 
Zanzibar kuendelea ni jambo jema, lakini kitendo cha mataifa ya nje kujinasibu kuwa yanapanga kuimarisha uhusiano wao na Zanzibar jambo ambalo ni kinyume na katiba ya nchi ni la kushitua.
Hakuna ubaya kama misaada hiyo itaisaidia Zanzibar.
 
Hakuna ubaya kama misaada hiyo itaisaidia Zanzibar.
Ni kweli, hakuna ubaya wowote kwa Zanzibar kupata misaada, lakini misaada hiyo pamoja mambo mengine kati ya nchi yetu na mataifa ya nje, vinapaswa kupitia / kufanywa na serikali ya muungano.
 
Mahusiano na mataifa ya nje ni jambo la muungano, linapaswa kusimamiwa na serikali ya Muungano.
Wewe si subiri wakija kwa mambo ya Muungano. Hao hawakuja kuhusi uhusiano wa mambo ya nje wala ya Muungano. Zanzibar ni nchi na ina Rais wake na hayo ni mambo yake ya ndani. Tanganyika ndio haipo.

Au wewe unajua zaidi ya Hussein Mwinyi na Samia Suluhu?
 
Zanzibar kuendelea ni jambo jema, lakini kitendo cha mataifa ya nje kujinasibu kuwa yanapanga kuimarisha uhusiano wao na Zanzibar jambo ambalo ni kinyume na katiba ya nchi ni la kushitua.
Naomba unukuu kipengele hicho cha katiba tafadhali.
 
Sawa ulosema.
lakini wengine ndio hawapendi na hasa viongozi wa CCM.
Maana hata hizo pesa tunazoomba msaada zikipita BOT basi hazitoki au zikitoka basi kazi kubwa sana na ugomvi.
Zile 4.5% za waZanzibari kutoa ka kwa JMT mapka leo hazikuja tnagu 1964.
Shirika la ndege la Tanzania linadaiwa Pesa nyingi kwa kutumia na kuegesha ndege kwenye Air port za zanzibar mpaka leo hawajalipa.
Lakini Zanzibar walitakiwa kukatiwa Umeme na Tanesco kutokana na madeni.

na mengine mengi tuu.
Ndio maana wa Zanzibri walio wengi hawautaki muungano huu uliopo
 
Tanganyika ipo imejificha chini ya jina la Tanzania.
 
Zanzibar iachwe angalao ipumue,kuimeza tumeshashindwa sasa tumuachie Mola atende yake.

Naona Mungu kapanga kuwa sisi ndio tumezwe na tuongozwe na Wazanzibari wenye kumuogopa Mungu.
Umeongea point halafu umepigwa ban! Jf bhana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…