SI KWELI Je, Marekani ni kosa kisheria kuvuna maji ya mvua?

SI KWELI Je, Marekani ni kosa kisheria kuvuna maji ya mvua?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu nimekutana na hii mtu kaandika huko X

"Inasemekana kuvuna maji ya Mvua ndani ya USA ni Kosa na unapigwa faini au kifungo.Mwenye anajua hii atuelezee please"
1773824403544.png
 
Tunachokijua
Kumekuwa na madai kwamba nchini Marekani hairuhusiwi kukinga maji ya mvua na ukibainika unaweza kufungwa ama kulipishwa faini.

Uhalisia wa madai hayo ni upi?

JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa hakuna sheria ya moja kwa moja inayowazuia wananchi wa Marekani kukinga maji ya mvua.

Tovuti ya rain water collector tanks kupitia makala yao ya mwaka 2021 wanaeleza kuwa hakuna sheria au kanuni za shirikisho (federal) zinazokataza watu kuvuna maji ya mvua. Ni majimbo saba tu ambayo yana vikwazo na/au yanahitaji vibali vya haki za maji kwa ajili ya uvunaji wa maji ya mvua.

Majimbo hayo ni Arkansas, Colorado, Kansas, Nevada, Oregon, Utah na Washington.

Ila kuna sheria tofauti na kanuni za uvunaji wa maji kulingana na jimbo husika kutokana na sababu mbalimbali. Yapo majimbo yanahamasisha watu kuvuna maji ya mvua kwa kuwaondolea kodi huku wengine wakiwa na sheria ngumu kidogo katika uvunaji huo.

Sababu zinazopelekea kuwepo kwa sheria za uvunaji wa maji ni:
  • Mahitaji ya Vibali (Permit Requirements)– Baadhi ya majimbo yanahitaji wamiliki wa nyumba kupata kibali kabla ya kufunga mfumo wa kuvuna maji ya mvua. Hii inaweza kujumuisha kuwasilisha mipango ya mfumo, kulipa ada, na kuhakikisha unazingatia viwango vya usalama.

    Haki za Maji (Water Rights) – Katika majimbo yenye sheria kali za haki za maji, maji ya mvua huchukuliwa kama sehemu ya rasilimali ya pamoja ya maji. Hivyo, wamiliki wa nyumba wanaweza kuwekwa mipaka kuhusu kiasi cha maji wanachoweza kuvuna.

    Viwango vya Ubora wa Maji (Water Quality Standards) – Majimbo mengi yana miongozo kuhusu kuchuja na kutibu maji ya mvua yaliyovunwa, hasa kama yatatumika kwa kunywa au matumizi ya nyumbani.

    Motisha za Kodi (Tax Incentives) – Baadhi ya majimbo kama Texas na Arizona hutoa punguzo au misamaha ya kodi kwa wamiliki wa nyumba wanaofunga mifumo ya kuvuna maji ya mvua. Motisha hizi husaidia kupunguza gharama za ufungaji.

    Vizuizi vya Matumizi (Use Restrictions) – Baadhi ya majimbo huruhusu matumizi ya maji ya mvua kwa shughuli zisizo za kunywa tu, kama umwagiliaji wa bustani, mapambo ya mandhari (landscaping), na matumizi ya chooni.


    Mifumo ya Lazima (Mandatory Systems) – Katika majimbo yenye ukame, kama New Mexico, baadhi ya majengo mapya yanatakiwa kujumuisha mifumo ya kuvuna maji ya mvua ili kusaidia uhifadhi wa maji.
Kwao maji ya mvua ni mali ya umma so huwa wanayaacha yaende msituni. Ukivuna kwa matumizi binafsi mtu akikuripoti unaweza kuchukukiwa hatua. Pia ni marufuku kuongea na Dolphins. Ukiongea nao au kufanya mazungumzo nao kuna Sheria inakataza.
 
Back
Top Bottom