Je! Mashine za kunyolea (za saloons) zinaweza kukuambukiza virusi vya UKIMWI?

nadhani kwa majibu tofauti yaliyotolewa tukiunganisha tunapata jibu sahihi
 
Uwezekano upo ila ni mdogo sana. Iekeweke kuwa HIV ni miongoni mwa virus dhaifu mno, kiasi ambacho vinaweza kufa hata kwa temperature ya 45°C. Pia hata vikipigwa na upepo kwa muda hata wa masaa 2 vikiwa nje ya mwili wa host, vinakufa pia. Inatakiwa muathirika awe na virus vingi mno ili aweze kumuambukiza mwingine kwa njia ya mashine za kunyolea tena muambukizwaji inatakiwa atumie soon baada ya muathirika kukatwa au kuchubuliwa na hiyo mashine. Na huyo muambukizwaji itabidi akatwe au achubuliwe pia.
 
MziziMkavu
@Decemption
Hawa jamaa wameniaminisha kuwa ngoma hamna, nimetafuta elimu binafsi na bado naendelea kuitafuta.... Ngoma inawezekana hamna hii kitu ni uzushi tuu. kama mliaminishwa eid amin nj mla nyama za watu basi mmeaminishwa kuna ngoma....

UKIMWI HAUPO JAMANI...
 
Haiwezi kwa sababu
(i) wembe wa mashine haukati kama kisu/panga ni kwa mfumo wa vibration ambapo virus hawawezi kuishi pale

(ii) Mashine huchemka haraka sna na kuzid jotoridi 36.94 km joto la binadamu hivyo kufanya wasiishi kwny joto kubwa

(iii) Kusafisha mashine kwa mafuta (eg spirti, etc) husababisha kuondoa kabsa vijimelea.
 
Saloon kunaile spirit inasaidia kufuta mashine kabla yakunyoa
 
Mmh ndio maana nanyoaga dongo na kiwembe tu au na mashine yangu binafsi home
 
Ingekuwa saloon kuna maambukizo hayo hadi leo hii sidhani kama JF ingekuwa na washiriki maana tungelishakufa wote humu...
 
Hii mada ya Mashine za saloon inazidi kunilegeza joint nikisubiria miezi mitatu nikapime ambapo salimika yangu ni Mungu aingilie kati.
 
Nadhani inawezekana. Umenikumbusha siku moja niligoma kunyoa baada ya kumuona mtu aliyenitangulia kunyoa akiwa na mapunye chungu nzima. Kinyozi alinihakikishia kwamba atasafisha vifaa vyake lakini nikamwambia nitaenda siku nyingine. Sijui hivi vifaa vyao wanavisafisha namna gani ili kuondoa uwezekano wa maambukizi kwa wateja wao.
 
Hatuwezi kukataa kabisa, possibilities zipo ila ni sisi kuangalia ni barber shops zipi zinazozingatia Infection Prevention Control measures kuna ambao wanasterilize shaving machines kila baada ya kumnyoa mteja na hii ndo njia kuu ya kuua vijidudu kwenye vifaa. Ila natoa angalizo tusisahau magonjwa mengine ambayo yanaambukizwa kwa njia hiyohiyo na yanauwa kwa kasi hata kuliko HIV eg Hepatitis B&C
 
Hii mada ya Mashine za saloon inazidi kunilegeza joint nikisubiria miezi mitatu nikapime ambapo salimika yangu ni Mungu aingilie kati.
Ingekuwa hivyo basi watu wote wanao nyoa salon wangekuwa na HIV
 
Thank you.

Hivi sasa sina wasiwasi sana pia ninatumia mashine yangu binafsi ya kunyolea.

I was affraid before. Kama mtu anaweza kupata vipele vya bakteria why Virus isiambukizwe. So kupitia research nimeanza kuelewa.

Thanks to all
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…