Binafsi huwa napata sana shida kubaini uwezo wa hawa watawala wetu kifikra katika kutatua matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii yetu. Kwa hivi sasa taifa letu limekumbwa na tatizo kubwa la anguko la elimu katika ngazi zote yaani elimu ya msingi,sekondari na hata elimu ya juu. Serikali kwa uzuzu au sijui kwasababu ipi inaamini kuwa kuchunguza tu ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha IV mwaka 2012 ndio mwarobaini wa tatizo hili. Hivi ni kweli kuwa tunaweza kutatua tatizo letu la elimu kwa njia hii pekee?