Habari bro
As I promised.
Nitakuwa hapa kujibu hoja zako always.
Hoja yako ni hii
Maandishi haya yanahoji kama Mathayo aliichukua aya ya Isaya nje ya muktadha na kuitumia kumhusu
Yohana Mbatizaji, ilhali Isaya alikuwa anaelezea ujumbe wake mwenyewe.
Mwenye ufafanuzi zaidi katika hili tafadhali njoo unisaidie.
Summary ya swali lako ni hii
1. Je? Isaya alikuwa anasema mwenyewe au alikuwa anamtabiria Yohana?.
2. Mathayo amesemaje kuhusu Yohana.
3. Au je? Isaya alikuwa anamsema yohana mbatizaji?.
Kwanza soma tena hili na Tuanzie hapa.
Isaya 40: 2-7
"2.Semeni na moyo wa Yerusalemu, kauambieni kwa sauti kuu ya kwamba vita vyake vimekwisha, uovu wake umeachiliwa; kwa kuwa amepokea kwa mkono wa BWANA adhabu maradufu kwa dhambi zake.
"Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya Bwana; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu.
4 Kila bonde litainuliwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patasawazishwa;
5 Na utukufu wa Bwana utafunuliwa, Na wote wenye mwili watauona pamoja; Kwa kuwa kinywa cha Bwana kimenena haya.
Inaendelea pia
6 Sikiliza, ni sauti ya mtu asemaye, Lia! Nikasema, Nilie nini? Wote wenye mwili ni majani, Na wema wake wote ni kama ua la kondeni;
7 Majani yakauka, ua lanyauka; Kwa sababu pumzi ya Bwana yapita juu yake. Yakini watu hawa ni majani.
8 Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele. "