Je, Matumizi ya kila siku ya Fridge, Blender, Pasi, Jiko la umeme n.k naweza vuka units 75 kwa mwezi?

Kwa fridge sio kweli...labda umemaansha freezer, unit 1.8 inatosha fridge ikiwashwa 24hrs labda hata kama imeinganishwa na freezer kdgo juu.inayokula umeme ni jiko LA umeme,pasi,kwa ulivyotaja labda uwe UMEUNGANSHWA KWENYE PHASE KUBWA YA KUPA 2.9UNITS KWA 2,000/-
 
Mkuu kwenye frij kama ukilitumia kwa umakini linaweza lisile sana umeme .mf huna haja ya kuwasha kama hujaweka vitu. Unakuta mtu kaweka maji lita 2 kaliwasha usiku kucha na mchan kutwa.
Jiko halina uhishi linakula hasa
Tv sio kivile labda pasi
Kweli nchi zetu ni za kimaskini. Friji isiyokuwa na kitu na mara nyingine inazimwa? Mimi nilidhani friji ni kitu cha kuwa ON 24x7 na unazima pengine wakati wa kuliosha tu!! Friji inawezaje kukosa kitu cha kuweka? Tena sehemu kama Dar?
 
Kuna rafiki yangu wamepanga wa 5 kwenye nyumba anasema wao kwa mwezi wanatumia umeme wa elf 4..

Hio suala nimekataa na sintokuja kuamini, labda kama huo umeme wanachajia simu tuu au Wanaiba, na nimemtishia kumshtaki Tanesco.
Huenda alinaanisha kila mtu kwa mwezi analipa hiyo elfu 4, ambayo kwa watu watano ni elfu 20 kwa mwezi
 
Mm huwa nanunua umeme wa buku 10. Napata units kama 70 na ushee. Huo umeme unakaa zaidi ya miezi 3 au miezi 4.
Hapo nina
fridge inawaka mda wote
Instant heater ua kuogea
Pasi napiga nguo za kazi daily for 5 days
Taa led ya nje watt 50 inakula umeme kiasi
Tv
Taa zinawaka mda mwingi sababu ndani giza
N.k nk
 
Na Mimi nakwambia! Fridge la watt 1000 haliwezi kutumia unit 1 kwa saa 12! Labda unaongelea DELI!
Hizo watt 1000 kitaalam maanake 1KWH Ambayo mtaani mnaita UNIT MOJA!
Hivyo kwa masaa12 haliwezi tumia unit moja ..Usiwe mbishi.
Maana yake linakula 1unit kila saa
 
Nina fridge ambayo inawashwa usiku kila siku kuanzia 12 jioni linazimwa saa 2 asubuhi nina taa 6 pasi inatumika kila siku Nina tv + radio matumizi kwa mwezi natumia tsh 40,000/ = ambazo napata units 112.
Wakati fulani gharama inaweza kuzidi au kupungua ila kiwastan gharama ni elf 40
 
Ndugu humu wakati mungine utadanganywa. Fuata maelekezo hapa chini:-
Kila kifaa cha umeme kina name plate ambako kuna maelezo ya ulaji wa umeme: mfano bulb ya 20W ikiwaka kwa muda wa masaa 50 ndipo inakula unit moja ya umeme yaani 1KWH
Maana yake unit moja ya umeme maana yake KWH 1.
Kwa hiyo chukua vifaa vyako vyote vya umeme, angalia kwenye nameplate utakuta kimeandikwa Wats zake ( Kilowats = Wats 1000), ukishajua hizo Wats za kila kifaa chako itakuwa rahisi wewe mwnyewe kujipangia utumie kwa muda gani ili ubaki kwenye mpango wako wa units 75 ambazo ni KWH 75.
Vivyo hivyo kifaa chako kwa mfano pasi ya 1500W ambazo hapa ni KW 1.5 ikitumika kwa muda wa saa moja itakula units 1500 Wat x 1 H == 1500WH au 1.5KWH
Nadhani itakusaidia kukokotoa mwenyewe mahitaji yako ya umeme kwa kila kifaa chako kwa muda maalumu.
 
Nina friji watts 1000,heater 2 za kuchemshia maji ya kuoga bafuni, pasi, tv na taa za kutosha. Nimejiunga tariff 4 nanunua unit 75 kwa mwezi kwa Tshs. 9150. Lakini mpaka nikifikia kununua tena nakuwa na unit kati ya 20 mpaka 30 zimebaki. Kuna wakati nilifikisha zaidi ya unit 200 nikakaa miezi 3 bila kununua na hazikuisha.

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Hiter,jiko,friji (frizer), hivyo tuu kama ni kila siku hata unity 100 hazitoshi kwa mwezi
 
Kwa ushauri jitahidi uweke na vya sola kama hiyo hiter na taa friji unaweza tutumia vya sola kidogo itasaidia
 
Umeetia chumvi sana mkuu nina friji , pasi,brenda na tv natumia unit 16.4 kwa week sawa na unit 65.6 kwa mwezi kwa sh 8,000. Sema matumiszi ndo shida unaweka maji lita 2 unawasha usiku kucha ...unaaliacha mchana kutwa linanguruma lazima lile sana.
Ukizima fridge na kuwasha unahisi ndo utapunguza matumizi? Mm sidhan navyofshamu fridge ulifikia ubaridi unaotakiwa inajizima yenyewe...au inajiweka katika hali ya kumaintain..Sasa iwapo utaizima ukija iwasha huoni kwamba utakua unaanza kazi upya ya kuanza kupooza vitu.
 
Nina fridge kubwa siiwashi masaa yote, Nina rice cooker, Nina jagi la umeme nachemshia chai tu, pasi, nina TV, ving'amuzi viwili, radio,blender watt 400 na taa sita, kwa mwezi sivuki unit 60, Tv yangu inch 32 watt 60. Rice cooker watt 700, jagi watt 2000 ila haizidi dakika tano nikichemsha maji, Matumizi yangu hayazidi Unit 60 kwa mwezi
 
Mkuu niunganishe na hiyo tarriff

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Halafu jua kabisa kama utanunua umeme mara mbili kwa mwezi ukiwa kwenye tarf 4 watakushusha kwenye matumizi makubwa tena zile unit 14 kwa 5000/= zitakuhusu. Over
Huo mwezi wanauhesabu vipi? Kila mwezi wa kalenda au kila baada ya siku 30?
 
Chukulia mfano kile kifridge kidogo kabisa cha mlango mmoja huwa kina watt 170w!
Kwa maana hiyo kwa saa moja kinabwia 0.17kwh, kwa masaa 12 kinakula unit 2.04kwh, kwa SAA 24 kinakulia Unit 4.08KWH
Mkuu upo serious kweli. Hivi unajua kinachokula umeme kwenye fridge ni compressor ambayo huwa inawaka na kuzima?

Mimi nina fridge la saiz ya kati nyumbani kwangu. Kukiwa na unit 1 nina uhakika wa kulala na kuamka niukute umeme labda utazima jioni.
 
Unaweza ukatoboa kama unajua mechanisms ya umeme inavyofanya kazi au kwa lugha nyingine katika nidhamu hasa hapo kwenye jiko na heater na inategemea ukubwa wa familia yako kwa maana kama una watoto wadogo inawezekana.

Mambo ya kuzingatia
Nunua taa 3 Watts achana na energy saver ambazo nyingi zina 11 watts, nakupa na mfano kabisa nyumba yako kama ina taa 10 za 3W ukawasha kwa masaa 10 zote kwa pamoja hizo taa zitatumia unit 0.3 yaani hata nusu unit hafiki na ukitumia taa 10 za energy saver zenye 11 watts utatumia unit 1.1 (hapo tayari umeona tofauti yaani taa za 3W ukiwasha masaa 10 zote kwa pamoja unatumia unit 0.3, wakati huo zikiwa za 11W unatumia unit 1.1 na kama ni taa za 5W utatumia unit 0.5)

Bana umeme kwenye matumizi ya taa maana watu wanadharau taa kumbe zinakula umeme bila kujua mfano tube light ondoa kabisa kama unazo mfano tubelight 1 ina 36 Watts hivyo ziwa taa 4 kama umeweka nje ukaziwasha kwa masaa 4 zitatumia unit kama 1.5 (moja na nusu)

Kwa taa za 3W na 5W zinatosha kabisa kutoa mwanga wa kutosha kwenye chumba cha kawaida ili umeme unao-save kwenye taa utumie kwenye hivyo vyombo vingine, Fridge haitumii umeme mwingi kama utakuwa unaiwasha kwa masaa kadhaa ili kama kuna ubaridi wa kutosha unazima hasa nyakati za usiku mnapoenda kulala alafu asubuhi unaliwasha kikubwa usitumie zaidi ya unit 2.5 kwa siku.
 
Hata taa zinaweza kula umeme. Mtu umefunga taa za watt 100 zipo 10 unategemea nini?
Umena mkuu watu wengi mechanism ya umeme inawasumbua, Hapa kwa saa moja tu hizi taa zinakula unit moja wakati kama umefunga za watt 5 zile LED zinakula 0.05 zinamwanga wa kutosha ni almost sawa na hizo za watt 100...sebuleni pale kama ni kubwa unahitaji mwanga wa kutosha hata kama kuna gipsum light zipo 4 bado unaokoa tu
 
Mkuu kwenye frij kama ukilitumia kwa umakini linaweza lisile sana umeme .mf huna haja ya kuwasha kama hujaweka vitu. Unakuta mtu kaweka maji lita 2 kaliwasha usiku kucha na mchan kutwa.
Jiko halina uhishi linakula hasa
Tv sio kivile labda pasi
Alafu kama issue ya maji ni kuweka kwenye Freezer juu ndani ya saa moja tu maji yamepoa kisha unazima
 
Ilo fridge la kutumia unit 4 Ni aina gani ?mimi natumia KIC nilinunua jipya kabisa linatumia unit 1 kwa siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…