Za jioni ndugu, nahamia sehemu, na sababu ni nyumba mpya Umeme Bado haujaunganishwa na zero taarifu, ila lengo langu nikitimiza masharti basi niunganishiwe ili niweze kuchezea kwenye units 75 kushuka maana nimesikia ndio kiwango cha juu kuunganishwa na zero taarifu.
Nilikotoka nilikua nimepanga, kwahio hata umeme ni wa share sikuweza ku calculate,
Sasa nitaanza kujitegemea, jee kwa watu wawili
Nikiwasha Fridge, Kupasi nguo asubuhi, Kutumia heater kupasha maji, Natumia jiko la umeme japo mara chache, Taa, Tv, radio, blender, breakfast Maker...
Je naweza fikisha pengine hata kuvuka matumizi ya units 75 kwa mwezi?
Kwa ufupi nina vifaa vingi vya umeme ila vya mara kwa mara ni hivyo, swali langu jee naweza kutumia units 75 kwa mwezi?
NOTE: vifaa vyangu vyote ni energy efficient.
Swali jingine la ziada, vigezo/taratibu za kuunganishiwa zero taarifu vipoje?
Na je katika zero taarifu 1,000tsh = units ngapi?