Je, Matumizi ya kila siku ya Fridge, Blender, Pasi, Jiko la umeme n.k naweza vuka units 75 kwa mwezi?

Safi yaani umeme ukioa kwenye taa hivyo vitu vingine unatumia vizuri bila shida
 
Ukihitaji Hiyo Utaambiwa Haipo
Nilifatilia Mizengwe Mingi Mpaka
Zipo ila wana discourage wanataka kuwapiga watu, mie kwa miaka 4 nimetumia huduma hii ila juzi kati mita iliharibika wakaniwekea mpya wakajifanya haipo, unachotakiwa ni kufuatilia kwa kupitia website yao watakujibu vizuri na hata humu Jamii Forum kuna uzi wa TANESCO kama matumizi yako kwa miezi 6 hayavuki unit 75 wanaweza kukuunganisha
 
Watu wengine bana eti lake linatumia unit 4 hehe usikute hana fridge anaongea tu
Watu hawajui Friji na pasi huwa zinajiwasha na kujizima hata kama pasi imeandikwa 1000W haina maana kwamba inawaka moja kwa moja au Friji kama limeandikwa watts kadhaa haina maana kwamba linawaka non stop. Kwanza friji za siku hizi zina raba kwenye milango ime-tight vizuri hivyo ubaridi unakuwepo wa kutosha
 
Mkuu kwanza nikupingeze kwa kujaribu kuhamia kwako.

Ila nikupe ujanja sijui kama utakuwa umeshauriwa tayari ama lah.
Mimi nilikuwa nalipa umeme mwingi sana.
Ile 10,000 napata units 28 na hii ni kwasababu yakufanya matumizi yakuzidi units 75 kwa Mwezi.

Nikaishirikisha familia yote kuhusu matumizi ya umeme, tukaamua kujicomit. Nikaongea na jamaa wa Tanesco akanirudisha Tariff 4 nikinunua wa 9,500 napata unit 75.
Ndani ya mwezi hatukutoboa licha ya kujibana sana.
Nikatumia ujanja, friji ikawa inawashwa mara moja kwa Siku.

Nguo zinapasiwa zote mara moja kwa wiki, no use of heater, no use of ricecooker ikawa hivyo ndani ya mwezi, tukabakiza unit 30. Tukaongeza 75unit mwezi uliofuata zikawa 105. Tukalegeza masharti, but bado zilibaki 40, mwezi uliofuatia tukanunua tena 75unit.
Zikawa zinaongezeka tu.

Huu ujanja ni mzuri unajitahidi kuzikusanya kwa miezi michache, baada ya hapo matumizi yako yanakuwa kawaida bila wasiwasi.
 
Sijajua mna kwama wapi, kwangu mpaka leo cjahamisha hiyo tarrif 4, nnalipa umeme wa 20,000 kwa mwezi ambayo ni unit 56 kwa mwezi, taa zangu zote ni LED, vyumban natumia watt 3, nje nmefunga watt5 mbele kuna watt7 uwanjani kuna watt 9 sebuleni natumia led za watt 12 ziko mbili, friji ninawasha usiku saa 3 hadi asubuhi, mchana inazimwa na inakaa na ubaridi mpaka jioni bila shida, tv natumia led ya inchi 32 ina watt 45 sina limit watumie vipi, jioni lazima wapike kwa rice cooker, nyama na maharagwe nk natumia electric pressure cooker. Fan zinatumika muda mwingi sasa nyie mnakwama wapi? Mtoa mada kwenye jiko la umeme siku shauri bora ununue induction cooker au hata infrared cooker na oven tumia microwave oven kama kweli una mpango wa kutumia umeme kupikia.
 
Unaweza ila utapika ugari mbich!
Suluari utanyoosha mguu mmoja tu!
Fridge utaiwasha kwa sekunde 100 tu
Taa utatumia mwanga wa tivi
 
Wanaotumia unit chini ya 75 kwa mwezi ni wale ambao maisha yao ni duni unakuta nyumba hiyo pasi hawana frige nayo hawana
 
Not real..!! embu waza hivi, friji used la 300W na Mpya la 1000W, unadhani lipi litakula umeme mwingi within the same time?
Heee!!we naye ni mtu wa ajabu!!unapolinganisha vitu, kuna mambo lazima uyazingatie!!anaposema hivyo ina maana chukua friji used la 300w, na then chukua friji jipya la 300w, ndipo utapata majibu!!sasa wewe unaleta mambo gani?!!
 
Niko nje kidogo ya mtoa mada. Mama angu yuko kijijini huko hakuna umeme wa tanesco. Kwa mwaka wastani anatumia umeme chini ya elfu kumi baada ya kumununulia Tv. Ila kbla ya kuwa na Tv ni elfu tano kwa mwaka.
 
Kwani Baba au Mama mwenye Nyumba hapo ulipopanga alikuambiaje kuhusu Mpangaji wake Wewe Kutumia sana Umeme na katika Kuchangia pale ukipigiwa Hodi Chumbani Kwako?
 
Mkuu unatumia friji gani au used?
Mimi natumi friji ya Boss auto ambayo hua inajizima baada ya muda flan inawaka yenyewe nikiiwasha bila kuzima 24 inkula unit 7, kimsingi huwa siizimi labda kama inafnyiwa usafi
Nina rice coocker inakula umeme kidogo sana kuivisha wali unit 0.5
 
Wanaotumia unit chini ya 75 kwa mwezi ni wale ambao maisha yao ni duni unakuta nyumba hiyo pasi hawana frige nayo hawana

Mkuu tumetumia pasi, birika na fridge na nyumba inawaka taa nje kama fuso (lori) na unit 75 haziishi kwa Mwezi (nyumba vyumba vya kulala vinne, sebule na jiko na dining. Watanzania wengi hata hao unaowaona sio duni wanatumia umeme chini ya unit 75 tatizo hawaelewi tu.

Mfano mtu amefunga taa 4 za tubelight nje (security light) anaziwasha masaa 12 anajikuta anatumia umeme unit 1.6 akichelewa kuzima asubuhi zinalimba unit 2 wakati mwingine anafunga taa 8 au hata 10 za LED za unit 5 yaani mwanzo wa kuta na mwisho (yaani taa 2 kila upande) na zinatoa mwanga wa kutosha kama tubelight na zipo 10 zinatumia nusu unit au chini ya unit 1 pamoja na kwamba ni nyingi
 

Upo sahihi watu wanatumia energy saver za 18Watts na Tubelight za 36watts au bulb za 40Watts wakiamini hazili umeme, kumbe kwa teknolojia ya zamani zilikuwa kweli nafuu ukilinganisha na bulb za 60W na 100Watts. Wanasahau ujio wa taa za LED mfano 5 Watts umepunguza matumizi kwa asilimia za kutosha mfano taa ya 60 Watts ukiiwasha kwa saa 1 itakula umeme sawa na taa 12 za LED za 5 Watts ambazo zitawashwa kwa saa 1 pia na mwanga ni mkubwa kuliko bulb ya 60Watts

[emoji115][emoji115]Hapo ndo wanapokwama
 
Hii kihesabu inakataa... Ila kiuwongouwongo inakubali...
kWh 1, ndiyo unit 1.... kWh = kW x hr
Sasa hiyo 1,000W, ni sawa na 1kW
Kupata kWh = 1kW x 12hrs = 12kWh

Hivyo kimahesabu, hilo fridge lako la 1000W, kwa masaa 12, litakula unit 12....

Ndio shida ya kununua fridge kwa kuangalizia kwa jirani (jokes), mtu ananunua fridge la 1000Watts wakati yapo mengi tu kwa matumizi ya kawaida ambayo yana nguvu chini ya 25% ya 1000Watts.

Watu waelewe wanaponunua vifaa vya umeme cha muhimu ni kuangalia “wattage” lakini pia fridge za siku hizi nyingi zina consumption ndogo za umeme na zinatambulika kama Energy star certified refrigerator”
 

Maelezo mazuri, mie huwa nawashauri watumie hizi taa za LED kwenye vyumba hapo kwenye mfano wako wa taa ya 20 Watts akitumia taa za watt 5 zitakuwa taa 4 ambazo akiziwasha masaa 50 atatumia 1 Unit

Watu wana nunua vifaa vya umeme pasipo kuangalia watt yake matokeo ana milki Tv la chogo la 150Watts alafu home kuna madogo hawana kazi ya kufanya Tv pekee inawashwa masaa 12 kwa siku unakuta Tv pekee inakula unit 1.8 ukichanganya na wananchi wengi wameaminishwa kwamba Tv haili umeme basi inakuwa tabu tupu
 
Tafuta pesa wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…