Je, matumizi ya mafuta kwenye Toyota Crown Athlete yapoje?

Baada ya kupitia mijadala mingi kuhusiana na huu mkoko nimeamua kwa dhati kabisa kujitosa kuuagiza used kutoka japan huenda muda mwingine uoga wetu tu unatufanya kushindwa kuwa na vitu vizuri.
Hio gari ni nzuri aisee, very comfortable hata kwa safari ndefu. Kwa wale tusio na uwezo na ma VX V8 ni mahala salama pa kupunguzia machungu. Crown ukijua kuiendesha haikutesi wala nini. Wanaoumia ni wageni wa magari😂
 
Unajua madalali hawana information kamili wanajazana ujinga kwa hearsays za vijiweni kisha wanawasokota sana wanunuzi hahah utaskia inakula mafuta sana hio chukua yenye 4 cylinder. Kumbe hawajui kinachobwia mafuta sio idadi ya Cylinder ni ukubwa wa cylinder. Zinaweza zikawa 4 ila ni mizinga ya cylinder😂😂😂

Ukiwa sio mjanja wanakutia mkenge!
 
Hio gari ni nzuri aisee, very comfortable hata kwa safari ndefu. Kwa wale tusio na uwezo na ma VX V8 ni mahala salama pa kupunguzia machungu. Crown ukijua kuiendesha haikutesi wala nini. Wanaoumia ni wageni wa magari[emoji23]
Ngoja nijilipue mkuu japo ndo itakua gari yangu ya kwanza ila nimefanya research na nimejiridhisha nimetoa uoga, maana nilikua na chaguo la Mark x kabla
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ngoja nijilipue mkuu japo ndo itakua gari yangu ya kwanza ila nimefanya research na nimejiridhisha nimetoa uoga, maana nilikua na chaguo la Mark x kabla
Its actually the same car but Crown iko na cosmetics zaidi. They share the same wheelbase, same engine ya 2.5L 4GR-FSE ila kwa CROWN imekuwa nyepesi zaidi. Ukitaka ma speed ipo vizuri sana ila pia ni gari ya heshima zaidi kuliko Mark X.
 
Ngoja nijilipue mkuu japo ndo itakua gari yangu ya kwanza ila nimefanya research na nimejiridhisha nimetoa uoga, maana nilikua na chaguo la Mark x kabla
ni chaguo zuri... hata mark X pia ni chaguo zuri

zinatumia same engine sema mark X imepitwa sehemu moja na crown

handling ya mark X kwenye kona ukiwa speed inahitaji uwe dereva haswa ila crown kwenye kona ukiwa speed iko very smooth

hapo tuuuu ndipo nilipoipaga maksi crown over mark x....

sisi wengine ni wazee wa mbio so huwa tunahitaji gari yenye stability kwenye hali zote

nilipigaga trip ya kusini na mshkaji wangu mimi nilikuwa na mark X yeye ana crown na zote tumefanya delimit so zilikuwa zinavuka 180kph na wote ni watu wakutembea

ila yeye ni muoga kidogo kwenye flat out nilikuwa namchapa ila kwenye kona yeye alikuwa anachukua point zote tatu
 
ni chaguo zuri... hata mark X pia ni chaguo zuri

zinatumia same engine sema mark X imepitwa sehemu moja na crown...
[emoji3][emoji3][emoji3] kwenye mbio hapo mie ni muoga mzee nadhani nikitembea sana 120. Thanx kwa experience yako mzee.

Pia mie siichukui kwa ajili ya safari ndefu ni mizunguko yangu tu na kwenda job basi hizo safari itokee mara moja moja tu
 
[emoji3][emoji3][emoji3] kwenye mbio hapo mie ni muoga mzee nadhani nikitembea sana 120 .
Thanx kwa experience yako mzee
Pia mie siichukui kwa ajili ya safari ndefu ni mizunguko yangu tu na kwenda job basi hizo safari itokee mara moja moja tu
safi sana mkuu ....na mbio sio nzuri na wala sikushauri sema tu ndio hivyo sisi wengine tulishakuwa maspeed adict

kwa hayo matumizi yako utadumu nayo sanaaa
 
Nafikiri alifaa aombe apewe ujuzi kuhusu hilo gari kwanza. Hii comment yako natumaini itampa mwangaza.
 
Mkuu umegonga kwenye mistari kabisa
 
Hahaha kuna jamaa yangu mmoja yeye ukimpa gari hua anasikia raha rpm akiifikia kwenye 3 yani nikiwaga nae nashangaaga sana aisee anapenda kuifanya gari ina scream yani yeye rpm inacheza 2300-3300 halafu gari auto yani naona hapa wese nililotia gari inachomwa vibaya..ila nilicho notice ni mfano ukiwa unakanyaga sana mafuta gia hua zinavuta sana ila ukiwa unakanyaga pole pole gia zonajibadili kiurahisi sana
 
Ile Altezza ya 3S ina 220HP mkuu
 
Eh ukilazimisha mzunguko mkubwa gia zinachelewa ku engage!
 
Weka 200,000.00 unaingia mjini...

Mkuu natofautiana na wewe. Binafsi nimeendesha mark X from Dar to Dodoma, then from dodoma to iringa kupitia mtera. Aisee mafuta ya 150K yalitosha kwa maana nilijaza mafuta nilipofika iringa. Nilipocheki odometer nilikuwa nimetembea karibu kilomita 800. So uendeshaji wa gari unamatter sana.

Ila kwa safari za mhini, same full tank inasogeza kilomita roughly 400 tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…