Je, Mayai ya kuchemsha yananenepesha?

Huo mchanganuo hata wenye sukari inawafaa waufuate
Wenye kisukari Wana sukari yao, diet nikupunguza kula sana yaani position ya chakula na siyo kupunguza makundi ya vyakula, wale wanaotumia protein nyingi kwa muda Fulani ni body builder maana protein inajenga mwili Sasa ukitaka nyama zihamie sehemu flani ndo unatumia protein huku ukizifanyia mazoezi zihamie hiyo sehemu ila Kuna protein nyingi Kila sehemu Kuna protein yake mfano protein ya kujenga nyama siyo protein ya kuzipa afya nywele.
 
Unene ni tumbo lililotanuka Sasa sijui utapunguaje kama tumbo lilishatanuka, ndo maana tunashauri ukinenepa punguza chakula na siyo kula kundi moja la chakula, wewe kula mayai yako hayo ila siyo Kila siku , kula makundi yote ya vyakula kwa kiasi kidogo kama utaweza kulizuia tumbo lako likishapata breakfast kiasi basi lisile hovyo hovyo tena mpaka chakula cha mchana na baada ya hapo chakula cha usiku kiasi, Sasa hapo unaona kiasi kwa Kila mlo na tumbo linabaki bila kuvimbiwa hata bia usivimbiwe maana ni wanga kama vyakula vingine, Sasa umesema diet, diet maana yake ni kula kwa afya yaani chakula cha makundi kiasi na chenye afya na siyo kuacha chumvi kabisa, kula chumvi kawaida ila acha sodium kama ajinamoto, sukari kiasi kama ukitumia Asubuhi basi vyakula vinavyofata unatumia bila sukari, chakula chako kiwe cha kupika mwenyewe Ili kuzingatia upishi wake mfano migahawa mingi Ili kuvutia wateja wanatumia ajinamoto Ili kufanya chakula kitamu, au kuivisha maharage na chakula haraka kwa baking powder na mara hamira kitu kinachofanya chakula kiondoke ubora wa afya na kipanue utumbo yaani unakula kupita kiasi na chakula hakikujengi kiafya unafutuka, ndo maana upike mwenyewe na uwe unanunua vitu vya afya, hiyo protein unayotaka ikufanye kupungua tumia butter siyo blueband, na jibini au cheese Ili kufanya wanga usilete shida ya obesity.
 
Karanga zina mafuta vitu km kashata ndio kabisa kuna sukar ba karanga ivo kwenye karanga bro umezingua ila apo kwenye mayai ya kuchemsha mmh na maziwa kizungumkuti
Hivyo vyote havina shida ukila kwa kiasi, labda maziwa fresh tu ndo ukishakuwa mtu mzima unatakiwa kula maziwa yaliyogoshiwa au kuchakatwa kama mtindi, butter ya maziwa na jibini ndo vinavyoweza kuchakatwa kwa mwili wa mtu mzima na kusaidia kuchakata wanga ndo maana nchi za wenzetu hutumia sana butter kupikia na miili yao ipo vizuri labda wale wenye kipato cha chini wasioweza kutumia na wale wanaopenda kula kupita kiasi yaani kikitokea chakula kitamu anakula mpaka hahemi na tumbo linatanuka kiasi cha kudai chakula kingi muda wote.
 
Siyo protein zote hasa protein ya mayai na nyama ya mafuta kupita kiasi lazima nyama ziongezeke.
 

Kwanza hongera kwa kufanya Diet. Ila pia Diet yako inafaa ifuate ushauri wa wataalamu, sio watu kama ulivyo sema. Kwa ufupi sana, ikiwa unataka kupunguza unene, basi fikiria namna ya kupunguza matumizi ya vyakula vyenye calories nyingi na ujihusishe sana na activities zenye kutumia calories maana calories ndo chanzo cha unene wako"
1. Sukari ni wanga, gramu moja ya wanga ina calories "4" so ikiwa unatumia sukari kwa kinywaji si shida, all you need ni kujua kiasi (gramu) za hyo sukari unazo tumia kwa siku. maana ukitumia gramu 250 tu tayari unakuwa na calories 1000, kama usipo zitumia kwa mazoezi au shughuli ngumu basi utazidi kuwa mnene.
2. Maziwa ni wanga pia (secondary sugar) hvyo kuna sukari ambayo huwezi jua ni kiasi gani, unaweza acha kutumia.

NB: Unaweza focus na matunda zaidi kuliko chakula chochote, nyama nyeupe sio mbaya, kama unatumia pombe acha kabisaaaa.... gramu 1 ni sawa na calories 8. Soda, juice za viwandani hizo zote piga chini. Nadhani kwa leo utakuwa umepata mwanga kidogo.
 
Watu theory ya kupungua hawaijui...
Ukitaka kupungua.. kata vyakula vyte vya wanga.. na sukari..

Ila kula vyakula vya protini na mboga mboga na mtunda.

Piga nyama kwa sana. Mayai. Yaan inshort kandaamiza nyama kama unaweza hata kila siku hunenep ngoo.. mchaw wa kunnenepesha ni mavyakula ya wanga.. ma mafuta. Kama unaweza kula nyama Isizo mafuta bas itafanikiwa

Wachina wanaongoza kwa kula nyama dunian na mboga mboga na hawal kabisa mafuta. .. si unawaona walivyo fit

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hebu nikusaidie ushauri maana mimi nilikuwa mnene ila nilifanikiwa kwa njia ya mtindi plain ambao ni low fat na punje 5 hadi 7 za vitunguu swaumu

Una kilo ngapi kwa sasa na una urefu wa sm ngapi?

Ulikuwa unakunywa mtindi na swaum kwa pamoja,?
 

Nyama haina mafuta?
 
Uko sahihi....nilikua na kg 98 now nina kg 80...nimeacha vyakula vya wanga na sukari...natumia matunda,mboga za majani,protin na ninakunywa maji ya kutosha kwa muda wa miezi mitatu...sasa nataka usipungue tena
 
ugali unanenepesha aisee hii si ni sqwq na kusema mahind yananenepesha fafanua mkuu ugali umeingiaje apo

Ugali ni wanga. Wanga ikizidi mwilini inazalisha Mafuta mengi yasiyo na kazi mwilini

Kinachonenepesha ni wanga Kwa sababu
Kwa hiyo kula ya kuchemsha tu

Protein hainenepeshi Sana ukilinganisha na wanga.
Weka wanga kidogo, mboga nyingi, matunda mengi, protein kiasi, maji Kwa siku Kita mbili na nusu mpaka tatu,
Usingizi usipungue masaa Saba.

Kula Milo mitano ukiwa umri miaka 2-6
Milo minne 7-13
Milo mitatu 14 - 30
Milo miwili 31 - 60
Milo mmoja 61-100
 
Kabisa...unajilia samaki mchemsho jion unalalia matango unapungua bila kukongoroka!
 
Huwezi wewe. Wenzio tumefanya sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…