Watalamu wa hizi kazi msaada tafadhali.
Nimekuwa nikijiuliza swali hili muda mwingi sana ila sipati jibu.
Imekuwa ni kawaida mtu kukatazwa kunywa maziwa pale tu pindi amezapo dawa kwakuwa huaminika kuwa maziwa huharibu dawa.
Sasa swali langu ni je,mtoto anaenyonya akipewa dawa hairuhusiwi kunyonyeshwa maziwa au mimi tu ndiyo sielewi?[emoji120]
Habari!
Ili kujibu vyema swali lako, ni vyema kuelewa kuwa maziwa ya mama ni sawa na maziwa mengine ila yanazidiana au kupungua kwa vitu vichache.
Kinacholeta shida kwenye maziwa ni muunganiko wa madini kama Calcium na Magnesium kwenda kwenye viambata vilivyoko kwenye dawa husika.
Uhusiano wa maziwa na dawa:
1: kuna dawa ambazo ukitumia, unahimizwa kutumia maziwa ili ziweze kufyonzwa vyema na hatimae kufanya kazi vyema.
2: kuna dawa ambazo haziathiriwi kwa chochote na maziwa.
2: kuna aina ya dawa ambazo ukinywa maziwa au ukinywa dawa husika, inakubidi usubiri kati ya saa 2 au zaidi ndo kingine kifuate. Hii hutokana na maziwa kutengeneza muunganiko ambao mwili hushindwa kufyonza. Dawa hizi ni kama
tetracycline, doxycycline, and ciprofloxacin nk.
Kwa ujumla dawa hizi hazitolewi kwa watoto wachanga. Ndiyo maana haya masharti hauyasikii sana kwa watoto.
NB: Ni wajibu wa mtoa huduma ya afya kukueleza haya kulingana na dawa alizokupatia, ingawa wakati mwingine ni muhimu kuuliza pia mahusiano haya kwa dawa alizopewa mtoto au mtu mzima.
Na hapa ndo tunasema, usikimbilie kumpa mtu aliyekunywa sumu maziwa. Kama sumu husika inayeyuka vyema kwenye maziwa basi utammaliza kwa simu kuyeyuka vizuri na kwenda mwilini.