1Afica54
Senior Member
- Feb 15, 2025
- 115
- 68
HABARI WANA JAMII FORUM
Naomba kuuliza kua kuna ukweli wowote juu ya mazoezi ya jelqing au Arabic milking ambayo yanadaiwa kuongeza ukubwa wa uume
Je kweli haya mazoezi yanafanya kazi?
===============
Daktari Rodolfo Favaretto anayehudumu kama daktari mkuu wa mfumo wa mkojo katika kituo cha huduma za afya Unidade do Convênio Prevent Senior/SP nchini Brazil anaelezea dhana ya kuongeza ukubwa wa uume kuwa ni suala ambalo mara nyingi wanaume hulichunguza ili kupata namna ya kufanikisha jambo hilo, hata hivyo, madaktari wa mfumo wa mkojo (urologists) hawapendekezi utaratibu huu unaofanywa na baadhi ya wanaume. Mbinu za kuongeza uume, kama vile pampu za kuvuta, pete za uume au dawa, hazijathibitishwa kisayansi na zinaweza kusababisha madhara kama vile maumivu ya kudumu, uharibifu wa neva, kutokea kwa damu kuganda, uharibifu wa tishu na matatizo ya nguvu za kiume.
Jelqing ni mbinu ambayo baadhi ya watu hutumia kujaribu kuongeza ukubwa wa uume. Huhusisha mazoezi ya kuvuta na kunyoosha uume, na mtindo huo umekuwa maarufu zaidi katika miaka ya hivi karibuni kutokana na ushawishi wa mitandao ya kijamii. Kitendo hicho husukuma damu kuelekea kwenye ncha ya uume. Pia hunyoosha tishu ndani ya uume na ngozi ya nje kwa lengo la kujaribu kuongeza ukubwa wake.
Kwa mujibu wa Rodolfo Favaretto ambaye ni daktari wa mfumo wa mkojo anasema ufanisi wa Jelqing haujathibitishwa kisayansi hivyo madaktari hawashauri matumizi ya njia hiyo aidha anaongeza kuwa kufanyika kwa kitendo hicho isivyostahili au mara nyingi zaidi kunaweza kusababisha maumivu,uharibifu wa tishu na matatizo ya nguvu za kiume.