Je, Mbunge mstaafu Upendo Peneza wa CHADEMA alibariki manunuzi ya gari ya DED kwa TZS 460 milioni?

Je, Mbunge mstaafu Upendo Peneza wa CHADEMA alibariki manunuzi ya gari ya DED kwa TZS 460 milioni?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kwa kawaida tumezoea kuwaona Wabunge na madiwani wa CHADEMA wakitoka mbele haraka haraka kutoa taarifa pindi wanapohisi kuna ufisadi kwenye maeneo yao.

Kwa mfano Devotha Minja wa Morogoro aliweka wazi ufisadi uliokuwa unafanywa kwenye ujenzi wa stendi ya msamvu wakati Rais Magufuli alipotembelea stendi hiyo.

Upendo Peneza alikuwa ni mbunge wa viti maalumu mkoa wa Geita na alikuwa diwani wa Geita kwa nafasi yake kama akina Msukuma na Kinyasu. Na wakati baraza la madiwani linapitisha ununuzi wa VX la DED kwa tsh 460,000,000.00 Upendo alikuwa barazani.

Je, kamanda huyu wa CHADEMA asiyekuwemo kule COVID-19 hakunusa ufisadi huu?

Maendeleo hayana vyama!
 
Rais Magufuli ametumia busara kubwa kwa hili na ameliacha libaki fundisho kwa watendaji wa serikali. Kwenye hayo manunuzi inawezekana kwamba taratibu zipo na zilifuatwa lakini viongozi hawakujiongeza kwanini gari la mil 460, hii ilikua ni muhimu.

Ingekua issue ya uwajibishwaji wengi wangewajibika kama DED mwenyewe
 
Tatizo lako wewe huwa hufatilii vyema yale yanayosemwa na wapinzani.
Kukuelewesha tu hapa.

Upendo Peneza alishalalamika sana bungeni kuhusu zaidi ya shilingi Bilioni 1.2 za halmashauri ya Geita kutumika pasipo kuwepo maelezo yoyote. Lakini kama alivyo ada, spika Ndugai alimfunga kinywa huku akimtaka akae chini tena kimya na hapo hapo Spika Ndugai kumpa hongera fisadi Jafo!

Yote kwa yote, shangingi la milioni 450 lilinunuliwa kwa baraka za ofisi ya waziri mkuu, hakuna kikao cha madiwani kilipitisha hilo.
 
Ulipaswa kujiuliza kwanza ni kwanini Magufuli hakumchukulia hatua Majaliwa wakati ofisi yake ilipoidhinisha ununuzi wa Shangingi la milioni 450 kwa DED wa Geita?
 
Hukumsikia Jaffo akisema haya yalifanyika baada ya bunge kuvunjwa?

Au umewasahau waliobakia ofisini hadi alipoapishwa jiwe?
 
Mnawauliza wapinga maendeleo? Hawa si kazi yao kupinga kila kitu? Au umesahau ghafla?

Hawa hawajawahi kuunga mkono jambo lolote, kwahiyo shikaneni uchawi wenyewe.

Ila nawaonya mkumbuke wakurugenzi ndio mitambo ya wizi wa kura, wakichoka kudhalilishwa watawaweka uchi namna mlivyoiba uchaguzi.
 
Nani alibariki wizi wa kura kwenye uchafuzi mkuu mwezi October? Maana hata mpinzani angepinga anakuwa 1 waliobaki wote ni kijani wa kugonga meza kuunga mkono kila kitu
 
Rais Magufuli ametumia busara kubwa kwa hili, na ameliacha libaki fundisho kwa watendaji wa serikali. Kwenye hayo manunuzi inawezekana kwamba taratibu zipo na zilifuatwa lakini viongozi hawakujiongeza kwanini gari la mil 460, hii ilikua ni muhimu....

Ingekua issue ya uwajibishwaji wengi wangewajibika kama DED mwenyewe
1.5trion ndiyo shida
 
Back
Top Bottom