Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
hivi ni klabu gani ilipewa mchezaji bure (kibabage) na Singida Black Stars ili awasaidie waondokane na umakolo waoKumekuwa na mjadala mkubwa miongoni mwa wadau wa soka nchini kuhusu uhusiano kati ya Young Africans Sports Club (Yanga) na Singida Black Stars, huku baadhi ya mashabiki wakieleza wasiwasi wao juu ya matokeo ya mechi kati ya timu hizo mbili.
Inafahamika wazi kwamba Yanga na Singida Black Stars wamekuwa na ushirikiano katika baadhi ya masuala ya soka, ikiwemo kuazimishana wachezaji au kufanya biashara za wachezaji. Pia, taarifa zilizowahi kujadiliwa na wadau wa soka zinaeleza kuwa kuna baadhi ya viongozi ambao wanahusishwa na pande zote mbili kwa namna moja au nyingine.
Hata hivyo, kinachozua mjadala zaidi ni mwenendo wa matokeo ya mechi zao katika Ligi Kuu Tanzania Bara. Baadhi ya wachambuzi na mashabiki wanadai kuwa katika mechi kadhaa zilizopita—zaidi ya tano—Singida Black Stars imekuwa ikipoteza dhidi ya Yanga, jambo linalowafanya baadhi ya wadau kuhoji kama kuna uwezekano wa kuwepo kwa makubaliano ya matokeo ili Yanga ipate alama sita kirahisi kila msimu.
Pamoja na hoja hizo, hadi sasa hakuna ushahidi rasmi uliowasilishwa unaothibitisha kwamba kuna upangaji wa matokeo kati ya timu hizo. Wapo pia wanaoamini kuwa hizi ni tuhuma zinazolenga kuchafua taswira ya Yanga, hasa kutokana na ushindani mkali uliopo kwenye soka la Tanzania.
Ahmed Ally ambaye ni meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba alionyesha kulalamika kwenye hili
Katika mazingira kama haya, jukumu la kuchunguza na kuthibitisha ukweli linabaki kwa mamlaka zinazosimamia soka nchini kama Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB). Taasisi hizi zina mamlaka ya kufuatilia tuhuma za upangaji wa matokeo na kuchukua hatua endapo kutabainika ukiukwaji wa kanuni za soka.
Mkuu wewe ni mtu wa mpira na hebu kuwa mkweli. Ukitoa simba na azam, team gani nyingine inaweza kuisumbua kabisa yanga hapa tanzania???Kumekuwa na mjadala mkubwa miongoni mwa wadau wa soka nchini kuhusu uhusiano kati ya Young Africans Sports Club (Yanga) na Singida Black Stars, huku baadhi ya mashabiki wakieleza wasiwasi wao juu ya matokeo ya mechi kati ya timu hizo mbili.
Inafahamika wazi kwamba Yanga na Singida Black Stars wamekuwa na ushirikiano katika baadhi ya masuala ya soka, ikiwemo kuazimishana wachezaji au kufanya biashara za wachezaji. Pia, taarifa zilizowahi kujadiliwa na wadau wa soka zinaeleza kuwa kuna baadhi ya viongozi ambao wanahusishwa na pande zote mbili kwa namna moja au nyingine.
Hata hivyo, kinachozua mjadala zaidi ni mwenendo wa matokeo ya mechi zao katika Ligi Kuu Tanzania Bara. Baadhi ya wachambuzi na mashabiki wanadai kuwa katika mechi kadhaa zilizopita—zaidi ya tano—Singida Black Stars imekuwa ikipoteza dhidi ya Yanga, jambo linalowafanya baadhi ya wadau kuhoji kama kuna uwezekano wa kuwepo kwa makubaliano ya matokeo ili Yanga ipate alama sita kirahisi kila msimu.
Pamoja na hoja hizo, hadi sasa hakuna ushahidi rasmi uliowasilishwa unaothibitisha kwamba kuna upangaji wa matokeo kati ya timu hizo. Wapo pia wanaoamini kuwa hizi ni tuhuma zinazolenga kuchafua taswira ya Yanga, hasa kutokana na ushindani mkali uliopo kwenye soka la Tanzania.
Ahmed Ally ambaye ni meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba alionyesha kulalamika kwenye hili
Katika mazingira kama haya, jukumu la kuchunguza na kuthibitisha ukweli linabaki kwa mamlaka zinazosimamia soka nchini kama Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB). Taasisi hizi zina mamlaka ya kufuatilia tuhuma za upangaji wa matokeo na kuchukua hatua endapo kutabainika ukiukwaji wa kanuni za soka.
Na je Simba ipo kwaajili ya kuipatia Yanga point ngapi?Hapo hakuna cha kuficha. Singida ipo kwaajili ya kuipatia Yanga point 6 na sio kushindania ubingwa.
This time around, wamezuga kufungia wachezaji wake wa 2 kwa makosa mbalimbali, ili kupunguza ushindani wa mechi na Yanga, baada ya hapo wamewafungulia kwa kujua mpinzani anaefuata ni Simba.
Nafikiri TFF haina meno katika ujinga kama huu. How come on earth mchezaji mwenye kosa la kupanga matokeo anafunguliwa kwa kuomba radhi?!
Kuna vitu vinatakiwa kufanyika tena kwa haraka kuondoa aina hii ya 'madudu' katika football yetu.
Angalau unaona hakuna jitihada zinazofanyika nje ya uwanja. Yanabaki matokeo ya uwanjani tu.Na je Simba ipo kwaajili ya kuipatia Yanga point ngapi?
Angalau unaona hakuna jitihada zinazofanyika nje ya uwanja. Yanabaki matokeo ya uwanjani tu.
Singida akifungwa na Yanga bila pilika za nje ya uwanja wala hakuna shida. Tatizo linakuja lazima kuwe na matukio tata ya kuwarahisishia Yanga kiwanjani.
Last year, walipumzisha wachezaji wa kikosi cha kwanza eti kwa madai ya uchovu, baada ya Yanga kushinda dakika za mwisho ndio wanaingia.
Huu ni UHUNI michezoni.