Je, Mhimili wa Bunge umemezwa na Mhimili wa Serikali?

Je, Mhimili wa Bunge umemezwa na Mhimili wa Serikali?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,842
Reaction score
31,076
Katika kipindi ambacho huwa kinatoka Live, kila siku ya alhamisi ya kila wiki, ambapo wabunge hupata wasaa wa kiuliza maswali ya moja kwa moja kwa Mheshimiwa Waziri mkuu

Moja ya maswali yaliyoulizwa leo ni kutoka kwa Mbunge wa viti maalum wa Chadema, Devotha Minja, ambaye aliuliza kuhusu mkanganyiko wa hizi chaguzi za Serikali za mitaa zilizopangwa na Serikali kufanyika tarehe 24 mwezi huu

Kwa hali ya kushanfaza sana, Spika wa Bunge letu, alimzuia Waziri mkuu asilijibu swali hilo, pasipo sababu za msingi

Ndipo hapo nikajiuliza hivi huu mhimili wa Bunge letu umemezwa na mhimili wa serikali?

Najua katika nchi yetu tunaendeshwa na msingi wa utawala bora, ambao mihimili yetu mitatu, ambayo ni Bunge, Serikali na Mahakama, vinafanya kazi kila mhimili kufanya kazi kwa Uhuru, katika kile kinachoitwa "check and balance"

Hivi tunaweza kuuita huo kuwa ndivyo ambavyo Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, inavyoelekeza?
 
Mystery,
Tanzania inaendeshwa na mhimili mmoja tu "uliojichimbia' wa Executive. Judiciary na Parliament ziko highly compromised. Hii ndiyo moja ya mapungufu makubwa matatu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Kama CJ angekuwa anapatikana independently kama wanajifanya Kenya basi Judiciary ingekuwa independent, kinyume chake CJ anateuliwa na Rais. Na kwa Rais wa sasa alimteua akamfanya kaimu CJ kwa miezi zaidi ya 6 kabla haja m-confirm. Kitendo cha kumfanya kaimu ilikuwa ni kumuambia kama utatekeleza ninacho kueleza nita ku confirm.

Spika wa Bunge anapatikana kutoka Chama chenye wabunge wengi bungeni. Haya nayo ni mapungufu ya Katiba yetu. Best practice ingefaa awe hana chama.
 
Kuna watu wanatafuta ardhi, mashamba makubwa, nashauri tutafute mtu wa aina hiyo mwenye uhitaji tupatane nae bei tumuuzie hili li-nchi lote, tugawane kilichopatikana kila mtu atafute ustaarabu wake, akatafute pa kwenda. Inawezekana ardhi hii ikatumika kama shamba la kulisha dunia
 
Naomba niweke sawa, Mh Mbunge wakati anauliza alikuwa anasoma kwenye karatasi wakati Kanuni zinasema maswali ya papo kwa hapo, kwa mujibu wa Itelijensia za Mh Spika alibaini swali lile alikuwa ameandikiwa, kabla hata hajamaliza kuuliza, ndio Mh Spika akamwambia arejee kanuni za kuuliza maswali kwa Mh Waziri Mkuu. Wala hajamkataza Mh Waziri Mkuu kujibu swali.
 
Mihimili mitatu ni kwenye maandishi tu lakini kiutendaji mhimili ni mmoja t ndio maana anaropoka kuwa hashauriki.
 
Back
Top Bottom