Katika kipindi ambacho huwa kinatoka Live, kila siku ya alhamisi ya kila wiki, ambapo wabunge hupata wasaa wa kiuliza maswali ya moja kwa moja kwa Mheshimiwa Waziri mkuu
Moja ya maswali yaliyoulizwa leo ni kutoka kwa Mbunge wa viti maalum wa Chadema, Devotha Minja, ambaye aliuliza kuhusu mkanganyiko wa hizi chaguzi za Serikali za mitaa zilizopangwa na Serikali kufanyika tarehe 24 mwezi huu
Kwa hali ya kushanfaza sana, Spika wa Bunge letu, alimzuia Waziri mkuu asilijibu swali hilo, pasipo sababu za msingi
Ndipo hapo nikajiuliza hivi huu mhimili wa Bunge letu umemezwa na mhimili wa serikali?
Najua katika nchi yetu tunaendeshwa na msingi wa utawala bora, ambao mihimili yetu mitatu, ambayo ni Bunge, Serikali na Mahakama, vinafanya kazi kila mhimili kufanya kazi kwa Uhuru, katika kile kinachoitwa "check and balance"
Hivi tunaweza kuuita huo kuwa ndivyo ambavyo Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, inavyoelekeza?