Naomba kuchangia hoja hapa:
Uzi huu si tu unaimiza mahakama kama muhimili wa taifa Kugoma hili kuhakikisha hukumu zake zinaheshimiwa lakini hapa tunapaswa kujiuliza swali la kikatiba ambalo ndilo linalopaswa kujibiwa sio kushinikiza chombo kidogo kilicho chini yake.
Swali la kikatiba ni
Je, Kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania ya mwaka 1977 kuna maaka yeyote iliyowekwa kwa dhumuni la usimamizi wa misingi ya taifa.? Yaani Mamlaka yenye kutoa tathmini na muongozo, mamlaka ya usimamizi wa ufuasi wa katiba, Mamlaka yenye kusimamia Uendelevu wa utawala wa sheria na mengineyo kama hayo.
Swali hili ndilo linaloleta utulivu wa kitaifa, na kwa ukweli kabisa Katiba ya mwaka 1977 imekaa kimya kuhusu swali hili zito na ijaweka mamlaka hayo kokote pale.
Naomba kupendekeza Rasimu ya katiba iliyo kwenye tovuti ya
www.katibampya.com ambayo yenyewe imeanzisha muundo wa dola lenye mihimili minne ya kitaifa, Yaani.
1.
BARAZA LA USIMAMIZI WA TAIFA (Muhimili wa usimamizi wa miaingi yote ya kitaifa, Mamlaka ya kimuungano kati ya tanganyika na Zanzibar, Mamlaka ya usimamizi wa ufuasi wa katiba, Tathmini, muongozo, mlinzi wa demokrasia, tunu za taifa, maadili ya taifa na mengineyo mengi.)
2.
SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. (Muhimili wa utendaji, utekelezaji wa sera za taifa, utekelezaji wa dira ya taifa ya maendeleo Endelevu na ustawi wa jamii, Ulinzi na usalama wa taifa na mengineyo kazaa.)
3.
BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. (Muhimili wa uwakilishi wa wananchi katika ngazi za majimbo, mamlaka ya kutunga sheria za nchi, Mamlaka yenye dhamana ya kujadiri muelekeo wa taifa na kupitisha bajeti na mengineyo kazaa.)
4.
MAHAKAMA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. ( Muhimili wa utoaji haki, hukumu za kisheria, mfasiri mkuu wa katiba na sheria, mtatuzi wa migogoro ya kisheria ya mihimili mingineyo na taifa zima kwa ujumla, na ndie mlinzi wa katiba kwa maana ya kuitafasiri au mamlaka yenye dhamana ya utafasiri wa mwisho wa katiba.)
Muundo huu unatoa jibu la maswali yote magumu ya kikatiba, pia katika hoja za uzi huu tunapata jibu kwamba vyombo kama magereza vitawajibika kwa baraza endapo tu wataonesha kutokutii takwa la mahakama kwa namna ambayo misingi ya utawala bora inadhoofika, yaani moja ya misingi ya utawala bora ni Utawala wa katiba na sheria. Hivyo basi baraza litasimamia misingi hiyo na kutoa muongozo kwa serikali au magereza wenyewe zaidi ya hapo baraza lina nguvu na mamlaka ya kuchukuwa hatua yeyote hile kwa maafisa wa magereza isipokuwa tu kwa kiwango cha usimamizi wa misingi ya taifa, yaani pale itakapothibitika misingi ya taifa inayohusishwa na mamlaka husika au chombo husika kwamba afisa au mtumishi husika hatekelezi wajibu wake ndani ya misingi hiyo.
Naomba niseme haya ili nieleweke vizuri. Changamoto kubwa ya kayiba yetu ya sasa imeweka kwamba Vyombo vya wananchi vipo chini ya Serikali pekee kama muhimili mkuu wa nchi na changamoto hii ndio inayopelekea mvutano huu. Hapa sasa ndipo Pendekezo la katiba lililopo kwenye tovuti tajwa linapata nguvu ya kweli na ya hali ya juu kwasababu imetamka kwamba mibimili yote ni sawa mbele ya taifa isipikuwa tu kwa Kanuni ya ulinganifu wa nguvu za mamlaka ya kikatiba, yaani
SURA ya kisheria iliyopo ndani ya sheria ya usimamizi wa taifa.
Katika rasimu hiyo Vyombo vyote vya wananchi vinawajibika kwa mihimili yote na vipo chini ya mibimili yote kwa mipaka iliyowekwa, yaani mfano Magereza
• itawajibika kwa
baraza kwa usimamizi wa misingi ya taifa, yaani chombo hicho kitende wajibu wake ndani ya misingi hiyo na mipaka yake.
• itawajibika kwa
serikali kifedha, sera na ulinzi.
• itawajibika kwa
Bunge kwa kutungiw sheria na utaratibu wa kujiendesha kwake.
• itawajibika kwa
mahakama kwa utafasiri wa sheria husika wanayoitekeleza (hapa ndipo mvutano wetu ulipo na hivyo kwa pendekezo la katiba lililopo kwenye tovuti tajwa linaliibua Baraza kuchukuwa hatua kwa magereza)
Naomba kuchangia hoja na kuwakaribisha kwenye kusoma Maoni yangu ya pendekezo la katiba kwenye tovuti ya
www.katibampya.com