Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Naamini Mbowe na Kisu kuna mchezo wanacheza baada yakuona CCM imepania kuondoa siasa za ushindani nchni
Ni miezi miwili sasa vyombo vya habari na wananchi wamejikita kufuatilia siasa za CHADEMA. Ni chama ambacho kimefanya mfumo wa uchaguzi uwe huru kuanzia kutangaza nia, kugombea na kushika madaraka. Ni chama ambacho viongozi wake pamoja na kupishana kisera na mitazamo majukwaani kimekuwa na nguvu ya umoja ndani jambo linalopelekea viongozi mahiri kusajiliwa kutoka chadema.
Ukubwa wa CHADEMA umepelekea CCM kutumia nguvu nyingi na fedha kwenda kuwanunua wanachama wa CHADEMA na kuwapa madaraka huku wana CCM wakiachwa bila kazi na uhuru wakusema.
Kwa mtizamo wangu , upo uwezekano mkubwa wa wana CHADEMA na mtandao wao wakawa watoa maamuzi ndani ya CCM na serikali. Upo uwezekano mkubwa wa CHADEMA kuongoza nchi kwa mwamvuli wa CCM.
Swali lakujiuliza, chadema inapata wapi nguvu na mikakati yakusajili wanachama wenye akili na vipaji? Nani anahusika kusajili wanachama hawa na anatumia mfumo gani? Leo kama Taifa kila kijana anaye hoji anaitwa activist au mwana CHADEMA. Najiuliza hawa CHADEMA wasio na fedha wala rasilimali wanawezaje kusajili na kuwatumia watu makini tofauti na CCM?
Mnakumbuka kikao cha CHADEMA nyumbani kwa Mbowe? Lisu na Mbowe wanacheza ngoma wanayoijua na wakimaliza kumpa Lisu Uwenyekiti Mbowe atakaa pale juu kama mshauri ila watakuwa wamekirejesha chama enzi za Slaa