Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,170
- 6,757
Kila mtu anajua kuwa mishahara ya watumishi wa umma ni midogo sana na kiuhalisia haikizi mahitaji ya kila siku.
Watanzania wengi wapo kwenye utumishi wa umma sababu tu ni ajira ya kudumu na ukiwa nayo kiasi fulani unaweza kupoza rim.
Hivi mtu anakuwa na net pay ya 350000 kwa maisha ya leo ataishi vipi? Kodi ya nyumba,chakula pamoja na ada za watoto!
Huyu ni mtu wa chini ambae nimetolea mfano, Je, hawa madaktari ambao wamekomaa mpaka wakawa wataalaamu wa kuokoa uhai wa watu,hata kama anapata mil 1.5 kwa maisha ya sasa bado ni pesa ndogo.
Je, kufanya kazi part time ili kujazia mapengo mshahara mdogo unaopata serikalini ni kosa? Je haiuruhusiwi kisheria? Mbona mawakili wengi wa serikali wanaofisi zao binafsi na wanapiga mpunga wa kugosha?kwa nini madaktari ndio mnawakaba roho wasitafute hata mkate wa ziada?
Watawala mtuhurumie basi.