Je, mimi kama mlipa Kodi naweza kumuagiza kiongozi kufanya jambo lenye manufaa kwa wananchi?

Je, mimi kama mlipa Kodi naweza kumuagiza kiongozi kufanya jambo lenye manufaa kwa wananchi?

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Naomba niulize, mimi kama mlipa Kodi siwezi kumuagiza Kiongozi yoyote afanye jambo ambalo ni faida kwa wananchi? Kama atafanya au kutofanya hilo ni suala jingine.

Sasa kama jamii ni vema kutumia rasilimali muda kujiuliza kwanini fulani amemuagiza Mtumishi wa Umma afanye hiki au kile au tujiulize kama kilichoagizwa sio kitu chema au hakina manufaa ya nchi?

Nadhani kama jamii tumekuwa tujikitiza kwenye technicalities badala ya ku-deal na big picture. Kwamba Katiba inanikataza mimi kumuambia Mtumishi wa Umma afanye hiki au kile? Yaani ninakatazwa mfano kumwambia Rais nampa siku nne Mgao wa Umeme uwe umeisha (Ofcourse huenda asifanye na asipofanya huenda sitampa Kura)? What's wrong with that?

Naona kama Taifa tumekuwa tukijikita kwenye petty issues kwa muda mrefu hivyo kupelekea mambo makubwa kutupita chini ya kapeti.
 
Mfumo! mfumo. Binadamu tunatabia ya ubinafsi. Nchi maskini tuna tabia za mtu maskini.
 
Mnashangaa Waziri Mkuu kuagizwa, mbona hata Mhe. RAIS huwa anaagizwa na Chama.

Kwamba kutokana na kero 1,2,3 za Wananchi basi uende ukashughulikie.

Though maagizo yao huwa kwa namna ya Kushauri na pia hutolewa Kwenye Vikao vya ndani vya Chama.

Alichofanya Mwenezi ni Kutafuta Kiki pamoja na Kujaribu kumueleza PM kuwa hatakiwi na hatokuwa Sehemu ya Serikali kuanzia 2025
 
Katiba ya Tanganyika iliyoasisiwa na Nyerere ndio root source ya yote haya.
 
Nadhani kama jamii tumekuwa tujikitiza kwenye technicalities badala ya ku-deal na big picture....; Kwamba Katiba inanikataza mimi kumuambia Mtumishi wa UMMA afanye hiki au kile ? Yaani ninakatazwa mfano kumwambia Rais nampa siku nne Mgao wa Umeme uwe umeisha ? (Ofcourse huenda asifanye na asipofanya huenda sitampa Kura)..., What's wrong with that ?
120909684_117545516779837_7410527070517376392_n.jpg

Wale wanaogonga meza kule saa hizi wanaasifu na kuabudu, lakini kiukweli Rais na wao waliomba kazi kwetu tukawapa ila tumejitoa ufahamu tunapigia magoti vyetu wenyewe
 
Attachments

  • 56917799_133229141170685_8438651898076069888_n.jpg
    56917799_133229141170685_8438651898076069888_n.jpg
    26.6 KB · Views: 2
Tatizo la nchi hii watu wake ni wajinga, "wajinga sana"; ndio maana hawawezi kutatua matatizo yao na ya watu wao kwa sababu wao wenyewe na hao watu wao ni wajinga sana.
 
Mnashangaa Waziri Mkuu kuagizwa, mbona hata Mhe. RAIS huwa anaagizwa na Chama.

Kwamba kutokana na kero 1,2,3 za Wananchi basi uende ukashughulikie.

Though maagizo yao huwa kwa namna ya Kushauri na pia hutolewa Kwenye Vikao vya ndani vya Chama.

Alichofanya Mwenezi ni Kutafuta Kiki pamoja na Kujaribu kumueleza PM kuwa hatakiwi na hatokuwa Sehemu ya Serikali kuanzia 2025
Point yangu ni kwamba hawa sio wafalme ni watumishi wetu.., hata mimi kama mlipa Kodi nina haki ya kumuagiza Rais matumizi ya Kodi zangu...

Nachoshangaa tunatumia rasilimali muda kwa kuanza ku-debate Haki ya mtu kuagiza (hata kama kisheria haipo lakini sioni tatizo la kumkumbusha mtu kazi yake) Kwahio cha maana sio nani ameagiza bali nini kimeagizwa...
 
Ni sahihi ila kuna namna ya uwasilishaji wa hoja kwa Viongozi wa Kitaifa.

Ndiyo maana pamoja na kulipa kodi zetu kwa Mamlaka lakini bado mkiwa na changamoto kama Wananchi mtalazimika kuiomba Serikali na sio kumuarisha Mhe. Rais

Sijui kama ni sahihi ama ni makuzi tuliyopewa dhidi Viongozi wetu wa Kitaifa
 
Back
Top Bottom