GE2025 Je, Misaada ya Kijamii Wakati wa Uchaguzi ni Njia ya Kununua Kura?

GE2025 Je, Misaada ya Kijamii Wakati wa Uchaguzi ni Njia ya Kununua Kura?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Wakuu

=====
hakuna lingine juu ya hii misaada

Wagombea siku hizi wamepata style mpya — wanabeba mabati, cement na hela, wanajifanya wanasaidia kujenga makanisa na misikiti. Ila ukweli ni kwamba, hiyo ni kampeni kwa kificho. Wanajificha kwenye imani ili wapate kura, alafu wanapiga picha na kupost wakidai "Mungu ameniongoza" — kumbe ni marketing ya kisiasa. Hii si sadaka, ni Unadanganywa bila kujua. Waumini wanapiga kura kwa emotions, sio hoja. Kura ya imani ikigeuzwa kuwa biashara ya kisiasa, basi tunaharibu uchaguzi mzima.

Soma, Pia: Kigoma: Rais Samia achangia TSh Milioni 50 Ujenzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Maria Mtakatifu Mwana wa Mungu
Rais Samia amechangia millioni 200 Ujenzi wa kanisa Kuu la Christ Cathedral Church, Dayosisi ya Mount Kilimanjaro
RC Njombe akabidhi shilingi milioni 30 kwa niaba ya Rais Samia, harambee ya ujenzi wa kanisa la Makao makuu (KKKT) - Dayosisi ya Kusini Kati

Kama kweli huyo mgombea ni mcha Mungu, mbona hakuchangia ujenzi wa kanisa au msikiti tangu awali?
Mbona misaada inatokea ghafla tu kipindi cha kampeni?

Ni kwa nini misaada kwa makanisa na misikiti huongezeka tu wakati wa uchaguzi?” Je, kutoa msaada wa kifedha kwa taasisi ya dini wakati wa kampeni ni kuvunja sheria za uchaguzi?
 
Huu ndiyo wakati wagombea wanatumia viinua mgongo vyao kutoa misaada na vijizawadi kwenye matukio yanayohusisha uwepo wa wananchi wengi ili kupata uungwaji mkono
 
Back
Top Bottom