Wagombea siku hizi wamepata style mpya — wanabeba mabati, cement na hela, wanajifanya wanasaidia kujenga makanisa na misikiti. Ila ukweli ni kwamba, hiyo ni kampeni kwa kificho. Wanajificha kwenye imani ili wapate kura, alafu wanapiga picha na kupost wakidai "Mungu ameniongoza" — kumbe ni marketing ya kisiasa. Hii si sadaka, ni Unadanganywa bila kujua. Waumini wanapiga kura kwa emotions, sio hoja. Kura ya imani ikigeuzwa kuwa biashara ya kisiasa, basi tunaharibu uchaguzi mzima.
Kama kweli huyo mgombea ni mcha Mungu, mbona hakuchangia ujenzi wa kanisa au msikiti tangu awali?
Mbona misaada inatokea ghafla tu kipindi cha kampeni?
Ni kwa nini misaada kwa makanisa na misikiti huongezeka tu wakati wa uchaguzi?” Je, kutoa msaada wa kifedha kwa taasisi ya dini wakati wa kampeni ni kuvunja sheria za uchaguzi?
Huu ndiyo wakati wagombea wanatumia viinua mgongo vyao kutoa misaada na vijizawadi kwenye matukio yanayohusisha uwepo wa wananchi wengi ili kupata uungwaji mkono