hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 13,628
- 20,992
Watawapokea Wapalestina wa Gaza
Wa kwanza ni Abdel Fattah El-Sisi, rais wa Misri, na wa pili ni Abdullah II, mfalme wa Jordan
Hawa jamaa ni pro west na pro Israeli. Walipokea misaada ya kutosha toka Marekani sasa na wao ni wakati wa kulipa. Wametakiwa kuwapokea wana Gaza milioni 1.5 ili kupisha ujenzi wa Gaza kwa miaka 5 ndipo warudi. Viongozi hawa wamekataa ombi hilo la Trump. Lakini Trump kasema atawafanya wakubali.
Naona watakubali
Aidha kwa hiari kwa njia ya ushawishi au kwa shinikizo wakikaidi. Maana Jordan ni ya pili baada ya Israeli kupokea misaada ya kiutu na kijeshi kutoka Marekani. Misri ikiwa ya tatu. Hivyo sio rahisi kumkatalia boss wako anayekulinda na kukupa lishe.
Nasaba zao
Sisi ni mtoto wa mama wa Kiyahudi kutokea Morroco na alipewa urais na Marekani baada ya kuagizwa ampindue Morse, rais halali aliyechaguliwa kidemokrasia. Kisha akamfunga jela kwa kitambo hadi umauti ulivyomfika kwa strock ya gafla akiwa mahakamani; wafuasi wake wanadai aliuawa. Morse alichukua msimamo dhidi ya Israeli na Marekani na west kwa ujumla, akitaka jeshi liivamie Israeli. Pia alitaka kuifanya Misri kuwa taifa la kislamu. Akatenguliwa kwa aibu kuu na mkuu wa majeshi wake ambaye ni El-Sisi. Tokea hapo akawa rais na kurejesha uhusiano na US na Israeli ambayo yalianza mnamo 1973 baada ya vita vya Yom Kipuri. Hivyo basi, El Sisi sio rahisi kumkatalia Trump. Maana anaweza kutolewa hapo.
Abdullah II, mama yake ni mzungu wa Uingereza, na wana majumba ya kifahari na hotel London. Na mfalme huyu amekulia uzunguni na anaishi kizungu. Na amezungukwa na washauri wa kizungu. Zingatia Uingereza ni pro zionism. Hivyo mfalme huyu hana baya na Israeli wala west, daima anailinda Israeli inaporushiwa makombora. Hivyo sio rahisi kumkatalia bwana mkubwa (Trump) maana anajua nini kitamfuata kama akikataa.
Benjamin Netanyahu
Juzi tarehe 4/2/25, Trump kampa rungu la mamlaka la kuwafukuza Wapalestina Gaza na maeneo atakayo, na kutokutoka kwenye maeneo yote aliyoteka. Kumbuka Trump ndio rais pekee wa US na duniani, kinagaubaga mnano 2017 october aliyetangaza kuutambua mji wa Yerusalemu kuwa mji mkuu wa Israeli. UN na mataifa yalipinga mpango huo, na Trump hakujali, alipeleka ubalozi wa US hapo hadi leo hivi. Hivyo hii ilidhihirisha uwezo na nguvu ya Marekani kidunia. Na sasa nguvu hii ipo nyuma ya Netanyahu na ndivyo serikali ya Wayahudi inataka pia. Maana maofisa wake juzi walijuzulu sababu ya Netayahu kukubali kusitisha vita baada ya serikali ya Biden kushinikiza amani. Sasa kichwa ngumu naam Trump ameunga mpango wa vita na kuahidi msaada mkubwa hata jeshi kufanikisha ajenda zote za Israeli hapo mashariki ya kati. Netanyahu akiitikia "naam" na kukukubaliana na mpango wa Trump wa kuikalia Gaza.
Hivyo inakuaje kwa Wapalestina?
Hawana chao hapo, wala hawana msaada wa hakika. Maana viongozi wa kanda yao hawana meno. Nani sasa mwenye meno makali ya kuwalinda? Ni Qatar? Hasha, huyo analindwa na US na kuna bezi kubwa sana ya US hapo. Labda mfalme Abdullah na Salman mwana mfalme wa Saudia? Mmmh hao ni walamba asali wakubwa, wapo bize kuifanya Saudia kuwa Dubai kuu kwa raha na anasa. Salman amekulia Ulaya ni msela nondo, anapenda wanawake na starehe. Daima anawaita wasanii wa kiume na wa kike kumuimbia na kuweka madisco kuwafurahisha vijana wa kiarabu (vizazi vipya). Kaifanya Saudia kuwa nchi ya kula Bata na ameapa kujenga Ulaya mpya ndani ya Saudia. Vijana wa kizazi kipya wa kiarabu, wanampenda kama nini. Si unajua tena hakuna asiyependa anasa duniani. Hivyo Wapalestina wamlilie Allah tu japo kawaacha kwa kitambo kirefu.
Lengo ya haya ni nini?
Ni kuigeuza mashariki ya kati na Afrika kaskazini kuwa nchi mfano wa Ulaya, zikiwa sio za kidini wala siasa kali. Na Israeli na Saudia zikiwa viongozi wa kanda hiyo. Jerusalemu kuwa jiji la kimataifa na Wayahudi kutawala eneo kubwa la mashariki ya kati kwa jina la kurejesha enzi ya mfalme Daudi ikiambatana na ujenzi wa HEKALU kubwa sana likiwa na ukumbi kwajili ya mataifa. Hekalu hili litafunguliwa na Waislamu, Wakristo, na Wayahudi. Watamachi siku ya ufunguzi huo kwa nyimbo ambazo zimeandaliwa tayari kuelekea hekaluni. Lakini ni kuhani mkuu tu wa Kiyahudi ndio ataingia hekaluni na kutoa kafara ya farakano kwa kumchinja Ng'ombe mwekundi kuwa kafara ya dhambi za Israeli na dunia. Mgeni rasmi atakuwa askofu wa Roma, na dunia itatangaziwa amani kuu na zama za millenia ya amani kuanza.
Haya yote yameshasainiwa na wakuu wa kiarabu na kislamu na wakuu wa wakristo na marabi wa kiyahudi. Hivyo wale ambao wanapinga, wataitwa washenzi na wavuruga amani. Na watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Angalia kwenye ajenda ya climate change, utaona viongozi wa dini zote walikutana, na wote wakimtukuza askofu wa Roma kwa mapendo yake ya amani ya dunia. Wote hawa wana lengo moja, kuifanya dunia kuwa kijiji cha amani. Kwahiyo Trump hakurupuki, alishapewa zawadi ya mzaituni wa amani na askofu wa Roma ili asisimamishe amani aidha kwa diplomasia au shinikizo.
Biblia inasema, "Hakuna amani kwa wabaya, asema Mungu wangu." Isaya 57:21. "Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa." 1 The 5:3 SUV
Na Jeff
Soma: Trump akazia, Jordan na Misri watawachukua wapalestina wa Gaza, mana US imewafanyia mengi