Wengi wetu tumewahi kusikia, kuuza ama kuvaa nguo zinazojulikana kama "mtumba", je umewahi kujiuliza hizo nguo zinatokea wapi.??
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2020 na mwandishi mmoja wa habari za uchunguzi nchini Finland, waligundua kwamba baadhi ya nguo ambazo wananchi wa taifa hilo wamekwisha zitumia na hazipo katika hali nzuri sana, huwa zinakusanywa na baadhi ya mashirika yakiwemo mashirika yanayotoa misaada mbalimbali nchini humo na mwisho wa siku mashirika hayo yanazisambaza nguo hizo katika nchi mbalimbali za Afrika na Mashariki ya kati. Ndo hizo zinaitwa "nguo za mtumba" kwa hapa kwetu.
Awali, mashirika hayo yalikana kusafirisha nguo hizo zilizokwisha tumika kwenda barani Afrika, lakini mwandishi huyo akaamua kufanya uchunguzi kwa kutumia vifaa maalumu vya ku"trak" mahali kilipo kitu ambapo aliweka vifaa hivyo kwenye nguo takribani 6 ambazo zilikwishatumika na kisha akazipeleka kwnye madustibin ambazo mashirika hayo yanakusanyia nguo "used"
Kwa mujibu wa mwandishi huyo, nguo zote zita zilisafirishwa nje ya nchi hio ambapo nguo moja ilikwenda nchini Ujerumani, nyingine Latvia na moja ilipoteza uelekeo kwahyo haikujilikana imeenda wapi.
Kuhusu nguo nyingine tatu zilizobakia:
Baada ya miezi mitano, kifaa kilichowekwa kwnye moja ya nguo kilisoma kipo nchini Nigeria.. Na baada ya miezi sita, kifaa kingine kilichowekwa kwnye nguo nyingine kilionesha kipo nchini Kenya na kubwa kuliko, nguo moja iliyobakia ilionesha imefika nchini Pakistani baada ya mwaka mmoja..
Huo ndo ukweli kuhusu nguo za mtumba