Je, mitumba ni nguo zilizochangwa ili kusaidia wasiojiweza?

Je, mitumba ni nguo zilizochangwa ili kusaidia wasiojiweza?

Mbona hata nje kwenyewe kuna maduka ya mtumba? Ushawahi kusikia dollar store?
 
Kibongo bongo tunaamini nguo za mtumba ni nzuri kuliko midosho ya special..
Wengi wetu tumewahi kusikia, kuuza ama kuvaa nguo zinazojulikana kama "mtumba", je umewahi kujiuliza hizo nguo zinatokea wapi.??

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2020 na mwandishi mmoja wa habari za uchunguzi nchini Finland, waligundua kwamba baadhi ya nguo ambazo wananchi wa taifa hilo wamekwisha zitumia na hazipo katika hali nzuri sana, huwa zinakusanywa na baadhi ya mashirika yakiwemo mashirika yanayotoa misaada mbalimbali nchini humo na mwisho wa siku mashirika hayo yanazisambaza nguo hizo katika nchi mbalimbali za Afrika na Mashariki ya kati. Ndo hizo zinaitwa "nguo za mtumba" kwa hapa kwetu.

Awali, mashirika hayo yalikana kusafirisha nguo hizo zilizokwisha tumika kwenda barani Afrika, lakini mwandishi huyo akaamua kufanya uchunguzi kwa kutumia vifaa maalumu vya ku"trak" mahali kilipo kitu ambapo aliweka vifaa hivyo kwenye nguo takribani 6 ambazo zilikwishatumika na kisha akazipeleka kwnye madustibin ambazo mashirika hayo yanakusanyia nguo "used"

Kwa mujibu wa mwandishi huyo, nguo zote zita zilisafirishwa nje ya nchi hio ambapo nguo moja ilikwenda nchini Ujerumani, nyingine Latvia na moja ilipoteza uelekeo kwahyo haikujilikana imeenda wapi.

Kuhusu nguo nyingine tatu zilizobakia:
Baada ya miezi mitano, kifaa kilichowekwa kwnye moja ya nguo kilisoma kipo nchini Nigeria.. Na baada ya miezi sita, kifaa kingine kilichowekwa kwnye nguo nyingine kilionesha kipo nchini Kenya na kubwa kuliko, nguo moja iliyobakia ilionesha imefika nchini Pakistani baada ya mwaka mmoja..
Huo ndo ukweli kuhusu nguo za mtumba
 
Na sisi end user utatusikia, VYA MTUMBANI UNAKUWA PEKE YAKO NA NI IMARA SANA
Of course nishawahi kuwa na bag moja la mtumba toka2012 limeibiwa mwaka huu

Lilikuwa kali sana 2020 ndo nilikuja ona mtu analo kama hilo nilshtuka sana hadi nikamfata nikamwambia πŸ˜† yeye pia alishangaa sana kama ninalo kama lile haamini kabisa langu siku hio niliacha na wote tumekutana tuko na baskeli
 
Unaona sasa wabongo sisi kwa ku-justify matumizi ya mitumba hatujambo
Vitu vipya kwa hapa kwetu vina kuwa havina ubora utakuta shati lime andikwa cotton lakini ukikishika siyo cotton, vilevile kwenye sandal ukinunua mpya utatumia miezi 6 zina katia tofauti na mtumba maana bidhaa za mtumba zinatoka dunia ya kwanza.
 
Mwa nilifika mitumba nanunua viatu haswa ila vya juu maana mwenyewe nilivaa siku mbili sina hamu na nguo hata iwe low quality napenda niivae mpya baada ya kufuata mara tatu sin hamu nayo ..
At least roho yangu inafurai siwezi kuvaa linguo mwaka mzima kwani uniform za shule kama pesa napata nguo kama chakula japo sio pesa ndefu sana ila kujipenda kila siku nguo mpya angalau naona nimejipa thamani angalau.
 
Back
Top Bottom