Mimi sio mwana sheria, nachojua yeyote yule aliyemtegemea huyo babu na mali yake katika maisha yake anahaki ya kupata urithi (kupata mgao)
Lakini pia mjukuu atapata mgao wa urithi kupitia kwa baba yake hata kama hayuko hai, kwa maana hiyo watoto hao 3 watagawana urithi bila kujali uhai wao.
MWISHO: USHAURI WANGU:
1.URITHI sio TUKIO ni Process (Ni namna gani ya kuziendeleza rasilimali alizoziacha
marehemu kwetu sisi na vizazi vijavyo)
2.URITHI: SIO kwa mtu mmoja (yaani mm juma nimerithi nyumba ya baba yangu)
HAPANA KABISA Juma anarithi na kizazi chake kupitia kwake ni mbio za kijiti ni lazima na yeye amrithishe mwanae na kuendelea
3. URITHI: SIO mali ya BAHATI HAPANA KABISA, Ni mali ya JASHO inastahili kuheshimiwa sio kamwe kuharibu au kuuza hovyo kama umeiokota vinginevyo hilo jasho la baba yenu ataliokota mtu mwingine baki kwa bei ya bure na lengo la baba yako litapotea nyie mtabaki maskini kwa maana hiyo bora yeye angeiuza kabla hajafa kuliko wewe.