Kennedy
JF-Expert Member
- Dec 28, 2011
- 54,894
- 64,043
Salaam Wa JF Wote
Nmekutana Na Mtu Mmoja Akiwa Anasumbuliwa Na Ugonjwa Wa UTI, Malaria, Kukosa Hamu Ya Chakula,Kwenye Maongezi Yetu Baada Ya Kumjulia Hali Akaniambia Ana Miaka 10 Hajawahi Kuugua Magonjwa Kama Malaria, UTI, Minyoo, Vidonda Vya Tumbo Na Magonjwa Mengi Mengine
Akaniambia Mwaka 2013 Alikwenda Safari Mombasa, Siku Moja Jioni Akaenda Ufukweni Mwa Bahari Kupunga Upepo Mwanana
Mzee Mmoja Akapita Na Ngamia Wake, Sasa Huyu Jamaa Alistaajabu Kuona Wanyama Wale Wakiwa Warefu Sana,
Akamfuata Mzee Anayewamiliki Aongee Naye Mawili Matatu Angalau Ajue Umri Na Namna Anavyowatunza. Anasema Hao Ngamia Walikuwa Na Umri Wa Miaka 15,Na Wanakula Aina Mbalimbali Ya Majani
Mzee Mwenyewe Ngamia Akamwambia Mkojo Wa Ngamia Unatibu Magonjwa Mengi Ya Binadamu Tena Haraka Sana, Jamaa Akasema Sasa Naupataje Huo Mkojo, Yule Mfugaji Akasema Anaongea Na Hao Wanyama Wanapokea Amri Na Kutekeleza Muda Huo Huo.
Jamaa Akaambiwa Tafuta Kopo Lete, Kwakuwa Ni Ufukweni Akapata Haraka Yale Ya Maji. Mfugaji Akaongea Na Mnyama Akakaa Chini Akampa Amri Atoe Mkojo Akatoa Wakakinga Lita Moja, Pia Watu Wengine Wakakinga
Baada Ya Pale Jamaa Akanywa Kama Nusu Lita Ya Mkojo Wa Ngamia Ilikuwa Mwaka 2013 Hakuwahi Kuumwa Malaria, Tumbo,Minyoo Na Magonjwa Yoyote Hadi 2023
Yeye Anasema Mkojo Aliambiwa Ndiyo Ulimsaidia
Nimeleta Maelezo Marefu Kiasi Nia Yangu Ni Kutaka Kujua Iwapo Kuna Mtu Yoyote Amewahi Kutumia Ama Kusikia Hili, Kwakuwa Tuna Ndugu, Jamaa Na Marafiki Wengi Wana Changamoto Mbalimbali Za Afya Na Wanatumia Gharama Nyingi
Naomba Kuwasilisha!!