Je, mkopeshaji anaweza kukamata mali ambayo mkopaji ameweika kama dhamana ya mkopo pasipo kupata idhini ya Mahakama?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Habari wadau,

Baadhi ya taasisi za kifedha zimekuwa na tabia ya kutishia ama kukamata mali ambazo wakopoja wameziweka kama dhamana.

Swali langu ni je, iwapo mkopaji atashindwa kilipa mkopo wake kama walivyokubaliana katika mkataba wa kukopeshana, mkopeshaji anaweza kukamata mali ya mkopaji iliyowekwa kama dhamana bila kwanza kupata idhini (hukumu) ya Mahakama?

Ukiacha swali hilo la msingi, nina maswali mengine kadha hapa chini:

Na je, vitu vya ndani kisheria vinaweza kutumika kama dhamana?

Kwa maneno mengine, mkopaji na mkopeshaji, wanavunja sheria kwa kutumia vitu vya ndani mfano radio, tv, friji, n.k kama dhamana?

Je, si kweli kuna sheria imezuia kutumia vitu vya ndani kama dhamana?

Na je, sheria hii inawatendea haki watu wasio kuwa na uwezo wa kuweka vitu kama hati za viwanja, magari, n.k, kama dhamana?

Majibu tafadhali.
 
Huo ni mkataba kama ilivyo mikataba mingine uliojaa haki na wajibu wa kila upande. Upande mmoja unapokiuka au kuvunja masharti, upande mwingine waweza kwenda mahakamani kusaka haki yake.

Hairuhusiwi kukamata mali bila kuihusisha mahakama. Kwanza, kila mkopeshaji lazima awe taasisi ya kifedha iliyosajiliwa na kufanya shughuli zake kisheria. Si kila mtu au kikundi cha watu kinaweza kukopesha. Haki za kimkopo zinapatikana mahakamani na si vinginevyo.

Kutegemeana na sheria na taratibu za taasisi ya fedha husika, vyombo vya ndani vinaweza kuwa amana. Wakati mwingine amana huwa ni ardhi, biashara, mali au hata mshahara. Amana ni kitu kinachowekwa rehani na mkopaji wakati wa kuchukua mkopo wake.
 
Ubarikiwe sana mtaalamu
 
Ukikopeshwa na bank utasaini mikataba kadhaa kutokana na rehani unayoiweka. Miongoni mwake ni chattle mortgage, legal mortgage, spouse consent, loan agreement nk.
Mikataba hiyo husainiwa kisheria na hupelekwa kwa msajili kubadilishwa jina na kuwa chini ya bank Hadi umalize mkopo. Kinyume na hapo bank in uwezo was kuuza iwapo hutolipa
 
Huo ni mkataba kama ilivyo mikataba mingine uliojaa haki na wajibu wa kila upande. Upande mmoja unapokiuka au kuvunja masharti, upande mwingine waweza kwenda mahakamani kusaka haki yake.

Hairuhusiwi kukamata mali bila kuihusisha mahakama. Kwanza, kila mkopeshaji lazima awe taasisi ya kifedha iliyosajiliwa na kufanya shughuli zake kisheria. Si kila mtu au kikundi cha watu kinaweza kukopesha. Haki za kimkopo zinapatikana mahakamani na si vinginevyo.

Kutegemeana na sheria na taratibu za taasisi ya fedha husika, vyombo vya ndani vinaweza kuwa amana. Wakati mwingine amana huwa ni ardhi, biashara, mali au hata mshahara. Amana ni kitu kinachowekwa rehani na mkopaji wakati wa kuchukua mkopo wake.
Halafu na madalali wa mahakama nao si wanatakiwa wasubiri hukumu ya mahakama kabla ya kukamata mali za mdaiwa?

Kuna jambo lilitokea mtaani kwetu sasa sikuelewa inakuaje madalali wa mahakama watishie kukamata mali za mdaiwa wakati mdaiwa hajawahi hata kuitwa mahakamani.

Kutojua sheria na taratibu kuna fanya wananchi wanyanyasike sana.
 
. Si kila mtu au kikundi cha watu kinaweza kukopesha. Haki za kimkopo zinapatikana mahakamani na si vinginevyo.
Asante Lawyer. Sasa hapo kwenye “sio kila mtu anaweza kukopesha” nina maswali mawili madogo ya nyongeza

1) Somebody X akimkompesha Mtu Y kwa maandishi kiasi cha pesa kwa masharti/makubaliano ya kulipwa pesa ile na certain % ya Riba baada ya muda flani then Y akadefault. Je, X anaweza kwenda mahakamani (au polisi kwanza) na kesi ikapokelewa na kusimama kwa kile kinachoitwa “kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu”?’

2) Kama jibu la swali la kwanza ni hapana, zaidi ya kukataa kutoa mkopo in the first place, lipi jingine ni jambo la msingi na lenye tija kufanywa na mtu X KABLA ya kuamua kumkopa Y (prevention) au baada ya aliyekopwa kudefault (fire fighting)?
 
Huo ni mkataba kama ilivyo mikataba mingine uliojaa haki na wajibu wa kila upande. Upande mmoja unapokiuka au kuvunja masharti, upande mwingine waweza kwenda mahakamani kusaka haki yake.

Hairuhusiwi kukamata mali bila kuihusisha mahakama. Kwanza, kila mkopeshaji lazima awe taasisi ya kifedha iliyosajiliwa na kufanya shughuli zake kisheria. Si kila mtu au kikundi cha watu kinaweza kukopesha. Haki za kimkopo zinapatikana mahakamani na si vinginevyo.

Kutegemeana na sheria na taratibu za taasisi ya fedha husika, vyombo vya ndani vinaweza kuwa amana. Wakati mwingine amana huwa ni ardhi, biashara, mali au hata mshahara. Amana ni kitu kinachowekwa rehani na mkopaji wakati wa kuchukua mkopo wake.
Nina nyongeza hapo msomi, kuhusiana na suala la taasisi pekee za kifedha zilizosajiliwa ndizo zenye mamlaka ya kukopesha tayari lilitolewa tafsiri na mahakama hivi karibuni kuwa tutajikita katika 'sanctity of contract' na tutazingatia lengo la awali la pande hizo mbili na kama consent ya mkopaji ilipatikana pasipo undue influence. Ninaperuze hapa, nikiipata hiyo case nitaiongeza hapa.

Pia kuhusiana na mdai kuweza ku'ceize mali ya mdaiwa ni kuwa hilo suala linawezekana kabisa kupitia doctrine ya bonafide claim of right japo tutapaswa kujuridhisha na mazingira ama situation ya tukio lote kwa ujumla kama kuna locus stand.

Asante
 
Asante Lawyer. Sasa hapo kwenye “sio kila mtu anaweza kukopesha” nina maswali mawili madogo ya nyongeza

1) Somebody X akimkompesha Mtu Y kwa maandishi kiasi cha pesa kwa masharti/makubaliano ya kulipwa pesa ile na certain % ya Riba baada ya muda flani then Y akadefault. Je, X anaweza kwenda mahakamani (au polisi kwanza) na kesi ikapokelewa na kusimama kwa kile kinachoitwa “kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu”?’

2) Kama jibu la swali la kwanza ni hapana, zaidi ya kukataa kutoa mkopo in the first place, lipi jingine ni jambo la msingi na lenye tija kufanywa na mtu X KABLA ya kuamua kumkopa Y (prevention) au baada ya aliyekopwa kudefault (fire fighting)?
1. Itategemeana na mlalamikaji anataka adai haki yake kwa namna gani. Endapo atapeleka suala polisi basi wengi hulenga kumkomoa mkopaji maana kesi hizo hata zikifika mahakamani na zikamalizika basi mtuhumiwa huishia(mara nyungi) kudaiwa faini ambayo huenda serikalini.
Lakini pia suala hili ukipeleka polisi itategemeana sana na askari atakayelipokea suala hili maana wengine hukataa na kueleza kuwa hayo ni madai na sio jinai hivyo mlalamikaji aende mahakamani kufungua shauri la madai.

Kubwa zaidi utambue kila mmoja ana namna na njia zake za kudai haki pale sheria inapomruhusu either kudai kupitia madai au jinai. Na kuna mwingine anaweza kuanza na jinai halafu anakupiga na madai juu.

2. Limejibiwa katika kipengele namba 1 hapo juu.
 
Hairuhusiwi kukamata mali bila kuihusisha mahakama.
Haki za kimkopo zinapatikana mahakamani na si vinginevyo.
Sio kweli, pindi mkopaji anaposhindwa kulipa mkopo, mkopeshaji anaruhusiwa kuuza mali ya mkopaji iliyowekwa kama dhamana moja kwa moja bila ya kupitia mahakamani. Anachotakiwa kufanya kabla ya kuuza ni kumpa taarifa ya siku 60 mkopaji kuwa asipolipa anachodaiwa, mali (nyumba) yake itauzwa. Na mnada unatakiwa kutangazwa walau siku 14 hivi kabla.
 
Nina nyongeza hapo msomi, kuhusiana na suala la taasisi pekee za kifedha zilizosajiliwa ndizo zenye mamlaka ya kukopesha tayari lilitolewa tafsiri na mahakama hivi karibuni kuwa tutajikita katika 'sanctity of contract' na tutazingatia lengo la awali la pande hizo mbili na kama consent ya mkopaji ilipatikana pasipo undue influence. Ninaperuze hapa, nikiipata hiyo case nitaiongeza hapa.

Pia kuhusiana na mdai kuweza ku'ceize mali ya mdaiwa ni kuwa hilo suala linawezekana kabisa kupitia doctrine ya bonafide claim of right japo tutapaswa kujuridhisha na mazingira ama situation ya tukio lote kwa ujumla kama kuna locus stand.

Asante
Hii ya kukopesha fedha, ukisoma hukumu ya Mahakama ya Rufaa haijaruhusu perse kuwa hata watu wasiosajiliwa wanaruhusiwa kukopesha kibiashara, kilichoelezwa ni kuwa nia ya mkopo inazingatiwa kama mkopo wenyewe haujakaa kibiashara.

Mfano, Katika kesi hiyo unayoizungumza, mkopaji alikopa Tshs. 2,600,000/= na kuahidi kuzirudisha kama zilivyo baada ya muda fulani, isipokuwa akishindwa kurudisha baada ya muda huo itampasa kurudisha na riba ya asilimia 30 kwa kila mwezi. Kwa hiyo hakukuwa na nia ya kibiashara tofauti na mkopo ungekuwa ni Tshs. 2,600,000/= inayotakiwa kulipwa baada ya miezi 3 ikiwa na riba ya asilimia 30. Hapo lazima leseni ya biashara ingehitajika.
 
Sio kweli, pindi mkopaji anaposhindwa kulipa mkopo, mkopeshaji anaruhusiwa kuuza mali ya mkopaji iliyowekwa kama dhamana moja kwa moja bila ya kupitia mahakamani. Anachotakiwa kufanya kabla ya kuuza ni kumpa taarifa ya siku 60 mkopaji kuwa asipolipa anachodaiwa, mali (nyumba) yake itauzwa. Na mnada unatakiwa kutangazwa walau siku 14 hivi kabla.
Una uhakika mkopeshaji anaweza kuuza mali iliyowekwa kama dhamana pasipo kwanza kwenda mahakamani?
 
Hii ya kukopesha fedha, ukisoma hukumu ya Mahakama ya Rufaa haijaruhusu perse kuwa hata watu wasiosajiliwa wanaruhusiwa kukopesha kibiashara, kilichoelezwa ni kuwa nia ya mkopo inazingatiwa kama mkopo wenyewe haujakaa kibiashara. Katika kesi hiyo mkopaji alikopa Tshs. 2,600,000/= na kuahidi kuzirudisha baada ya muda fulani, isipokuwa akishindwa kurudisha baada ya muda huo itampasa kurudisha na riba ya asilimia 30 kwa kila mwezi. Kwa hiyo hakukuwa na nia ya kibiashara tofauti na mkopo ungekuwa ni Tshs. 2,600,000/= inayotakiwa kulipwa baada ya miezi 3 ikiwa na riba ya asilimia 30. Hapo lazima leseni ya biashara ingehitajika.
Hii ina utata kama 2.6 mtu anafail je plus riba hii inakuaje mahakama inabariki hili? Mwamba umeua hapa
 
Habari wadau,

Baadhi ya taasisi za kifedha zimekuwa na tabia ya kutishia ama kukamata mali ambazo wakopoja wameziweka kama dhamana.

Swali langu ni je, iwapo mkopaji atashindwa kilipa mkopo wake kama walivyokubaliana katika mkataba wa kukopeshana, mkopeshaji anaweza kukamata mali ya mkopaji iliyowekwa kama dhamana bila kwanza kupata idhini (hukumu) ya Mahakama?

Ukiacha swali hilo la msingi, nina maswali mengine kadha hapa chini:

Na je, vitu vya ndani kisheria vinaweza kutumika kama dhamana?

Kwa maneno mengine, mkopaji na mkopeshaji, wanavunja sheria kwa kutumia vitu vya ndani mfano radio, tv, friji, n.k kama dhamana?

Je, si kweli kuna sheria imezuia kutumia vitu vya ndani kama dhamana?

Na je, sheria hii inawatendea haki watu wasio kuwa na uwezo wa kuweka vitu kama hati za viwanja, magari, n.k, kama dhamana?

Majibu tafadhali.
Hii mada ni moto na janga la kitaifa kwa sasa
 
Una uhakika mkopeshaji anaweza kuuza mali iliyowekwa kama dhamana pasipo kwanza kwenda mahakamani?
Nina uhakika mkuu.

Sheria ya Ardhi Sura ya 113 imeeleza hivyo kupitia kifungu cha 126 (kama dhamana ni nyumba). Hapitii kokote kule zaidi ya tu kukupa taarifa mkopaji kuwa atauza nyumba
 
Hiv mkopo inatakiwa uwe mkubwa kuliko dhamana,au dhamana iwe kubwa kuliko mkopo??
 
Nina nyongeza hapo msomi, kuhusiana na suala la taasisi pekee za kifedha zilizosajiliwa ndizo zenye mamlaka ya kukopesha tayari lilitolewa tafsiri na mahakama hivi karibuni kuwa tutajikita katika 'sanctity of contract' na tutazingatia lengo la awali la pande hizo mbili na kama consent ya mkopaji ilipatikana pasipo undue influence. Ninaperuze hapa, nikiipata hiyo case nitaiongeza hapa.

Pia kuhusiana na mdai kuweza ku'ceize mali ya mdaiwa ni kuwa hilo suala linawezekana kabisa kupitia doctrine ya bonafide claim of right japo tutapaswa kujuridhisha na mazingira ama situation ya tukio lote kwa ujumla kama kuna locus stand.

Asante
maelezo naona ni mazuri lakini yanawasaidia nyinyi tu wasomi maana mnaongea lugha zenu za kisheria badala kunyumbulisha na si std7 tukaelewa!!!! elezeni kwa lugha rahisi tuelewe wote
 
Back
Top Bottom