Je mlalamikaji yupo sahihi??

Je mlalamikaji yupo sahihi??

T-Bagwell

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2017
Posts
1,243
Reaction score
2,378
Habari za muda huu wana JF??

Nimekutana na video moja mitandaoni iliyorekodiwa na muumini wa dini ya Kiislam akilalamikia Kanisa lililopo karibu na Msikiti alipokua anakwenda kufanya ibada na kukuta Redio ikiwa inaimba kwaya Kanisani hapo pasipo kuwa na mtu ndani.

Muumini huyo amelalamikia na kuziomba mamlaka kuingilia kati swala hilo kutokana na kile alichokua anakilalamikia.

Mimi sio muumini wa Imani hizo mbili tofuauti(Ukristo na Uslam)

Baada ya kufuatilia comments kwenye post hizi nimeona waumini wa Imani hizo tofauti kila mmoja akitetea upande wake.

Kwa upande wangu na kuheshimu Imani hizo nimeona wote kwa wakati huo walikua na makosa

1. Kanisa limefungulia kwaya kwa sauti kubwa inayoweza kuwafikia na kuwakwaza hata waumini wasiokua waumini wa Imani hiyo au waliopumzika jirani na maeneo hayo,

2. Msikiti umefungwa speakers nje na inasikika adhana kwa sauti kubwa kitu ambacho pia kinaweza kuwa kero kwa wasiokua waumini wa Imani hiyo.
 
Attachments

  • Snapinst.app_video_AQOfZUCRvC40rkoW8EGMcp9uBADefFujQVGQ7fYun7fzzk-TuDb9fpPCriRtgKZ5945xzvve64R...mp4
    8.6 MB
Eti "Potential for conflict "....Foolish!
Fanya yako..msikiti upo wazi ingia kasali then tokomea....Huyu anawashwa
 
Hakuhudhuria mdahalo ? both Jesus and Muhammad are brothers in faith
 
Habari za muda huu wana JF??

Nimekutana na video moja mitandaoni iliyorekodiwa na muumini wa dini ya Kiislam akilalamikia Kanisa lililopo karibu na Msikiti alipokua anakwenda kufanya ibada na kukuta Redio ikiwa inaimba kwaya Kanisani hapo pasipo kuwa na mtu ndani.

Muumini huyo amelalamikia na kuziomba mamlaka kuingilia kati swala hilo kutokana na kile alichokua anakilalamikia.

Mimi sio muumini wa Imani hizo mbili tofuauti(Ukristo na Uslam)

Baada ya kufuatilia comments kwenye post hizi nimeona waumini wa Imani hizo tofauti kila mmoja akitetea upande wake.

Kwa upande wangu na kuheshimu Imani hizo nimeona wote kwa wakati huo walikua na makosa

1. Kanisa limefungulia kwaya kwa sauti kubwa inayoweza kuwafikia na kuwakwaza hata waumini wasiokua waumini wa Imani hiyo au waliopumzika jirani na maeneo hayo,

2. Msikiti umefungwa speakers nje na inasikika adhana kwa sauti kubwa kitu ambacho pia kinaweza kuwa kero kwa wasiokua waumini wa Imani hiyo.
Ustaarabu umekosekana hapo.
Zipo Sehemu Nyingine Huwa wanaheshimiana na Kusalimiana Kwa Furaha.
. . . . Hao Viongozi wa Hayo Madhehebu Wote wapelekwe SHULE YA UONGOZI wakafunzwe MAADILI.
 
Mbona hata ule mdomo wa bata huwa unaongeaga usiku kucha na tena vitu visivyo eleweka .............mara kitanda chako ndio kaburi shuka yako ndio sanda.............mbona huwa atuongei kitu.......kwanini msiwaambie tu waumini wenu humo humo msikitini kimya kimya bila kelele kwa kira mtu??
 
Habari za muda huu wana JF??

Nimekutana na video moja mitandaoni iliyorekodiwa na muumini wa dini ya Kiislam akilalamikia Kanisa lililopo karibu na Msikiti alipokua anakwenda kufanya ibada na kukuta Redio ikiwa inaimba kwaya Kanisani hapo pasipo kuwa na mtu ndani.

Muumini huyo amelalamikia na kuziomba mamlaka kuingilia kati swala hilo kutokana na kile alichokua anakilalamikia.

Mimi sio muumini wa Imani hizo mbili tofuauti(Ukristo na Uslam)

Baada ya kufuatilia comments kwenye post hizi nimeona waumini wa Imani hizo tofauti kila mmoja akitetea upande wake.

Kwa upande wangu na kuheshimu Imani hizo nimeona wote kwa wakati huo walikua na makosa

1. Kanisa limefungulia kwaya kwa sauti kubwa inayoweza kuwafikia na kuwakwaza hata waumini wasiokua waumini wa Imani hiyo au waliopumzika jirani na maeneo hayo,

2. Msikiti umefungwa speakers nje na inasikika adhana kwa sauti kubwa kitu ambacho pia kinaweza kuwa kero kwa wasiokua waumini wa Imani hiyo.
Kama ni eneo la makazi. Msikiti na kanisa havipaswi kuwepo hapo.

Jambo la pili huu ni udhaifu wa mamlaka husika. Nafikiri ofisi za mipango miji

Hv siku hizi hakuna askari wa ardhi!!???

Lkn pia niongeze kwa kusema hizo pande mbili zingeungana kiwe kitu kimoja ingekuwa furaha ilioje
 
Ukisikiliza kwa makini utagundua sauti inayosikika zaidi ni ile inayotokea msikitini. Maana wao wameweka kipaza sauti juu hivyo sauti kwenda mbali zaidi ukilinganisha na kanisa walio fungulia kwaya inayosikika kwa mbali kutoka kwenye spika
 
Nani aliyemkuta mwenzie, tuanzie hapo kwanza.
Ukiangalia kwa makini ni kama kanisa ndio lilitangulia kwasababu hata majani yameshaota pembeni tofauti na msikiti ambao bado unaonekana ni mpya.
 
Vyote vivunjwe, waumini wa pande mbili zote wanyongwe.
Suluhisho ya kishujaa hii. Kunogesha zaidi, wajenge bonge moja la bar na ukumbi wa disco kwenye hivyo viwanja.

Hapo utaona mashehe na mapadri wote wakijumuika kusaga rhumba.
 
Back
Top Bottom