Je, Mmeru na Mwarusha ni kabila moja?

Je, Mmeru na Mwarusha ni kabila moja?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Hawa ni watu wa wapi?

Nilijaribu kufatilia wameru ni kweli wanasikilizana na wamachame wapo tofaauti na wachaga, nadhani ni ni wamasai walioamua kuhamia Machame, hupenda kubeba visu na pia kibiashara bado wana mwamko mdogo.

Kwa Mwarusha nae naona wanatahiri kama wamasai na kuna fimbo za bomani kama wamasai.

Waarusha na wameru ni kabila moja?

Asili yao wote ni wamasai?
 
Kabila tofauti.
Mchaga wa Machame na Mmeru wamepakana na wana vinasaba vya kindugu lskini ni kabila tofauti.

Hata hivyo hata wakibosho, wa uru, marangu baadhi ya maneno wanasikilizana na wameru.

Mwarusha na mmeru hawasikilizani na hawapendani ) wanadharauĺiana)

Mwarusha ni mmasai wa mjini.

Wanasikilizana na wamasai wa porini na majina yao ni yale yale Laiza, Molleli nk
 
Kabila tofauti.
Mchaga wa Machame na Mmeru wamepakana na wana vinasaba vya kindugu lskini ni kabila tofauti.

Hata hivyo hata wakibosho, wa uru, marangu baadhi ya maneno wanasikilizana na wameru.

Mwarusha na mmeru hawasikilizsni na hawapendi pia.

Mwarusha ni mmasai wa mjini.

Wanasikilizana na wamasai wa porini na majina yao ni yale yale Laiza, Mileli nk
Wamasai na Waarusha ni makabila mawili tofauti japo wanasikilizana lugha.

Wameru na Wamachame wanaelewana lugha japo ni makabila tofauti.

Kimsingi, miongoni mwa makabila makuu (siyo pekee) Arusha ni Wameru, Wamasai na Waarusha.

Hayo makabila matatu yana baadhi ya desturi wanazoshea lakini kila moja lina upekee wake unaolitofautisha na jenzake.
 
Naamini zaidi hii post kuwa muarusha ni mmasai part 2
 
Wamasai na Waarusha ni makabila mawili tofauti japo wanasikilizana lugha.

Wameru na Wamachame wanaelewana lugha japo ni makabila tofauti.

Kimsingi, miongoni mwa makabila makuu (siyo pekee) Arusha ni Wameru, Wamasai na Waarusha.

Hayo makabila matatu yana baadhi ya desturi wanazoshea lakini kila moja lina upekee wake unaolitofautisha na jenzake.
Mpaka kesho siamini kama kuna kabila linaloitwa Muarusha,

Nnachofaham mimi Arusha ina makabila makuu mawili
, Masai na Chaga

Hawa wamasai ,kwa hapo arusha wamegawanyika mara mbili kuna wa mjini ambao ndo hao mnawaita waarusha na kuna wale wa ndanindani lakini wote ni wamasai

Ukija upande wa pili, hawa wanaoitwa wameru kiasili ni wachaga wa machame waliohama kutafuta maeneo miaka hiyo ndo wakaanzisha makazi yao huko meru, ila baada ya miaka kupita na muingiliano.wa jamii ya wamasai na wachaga ndo wakaform hao wameru ,na ndo maana mmeru anatabia zote mbili za kimasai na za kichaga

Kwa lugha rahisi mwenye asili ya Arusha kabisa ni Mmasai peke yake, haya makabila mengine yamekuja tuu

Kingine msichofahamu ni kwamba , Mchaga wa machame, Mmeru na Mkikuyu wa kenya wote wanasikilizana

Sent from my SM-A235F using JamiiForums mobile app
 
Hawa ni watu wa wapi?

Nilijaribu kufatilia wameru ni kweli wanasikilizana na wamachame wapo tofaauti na wachaga, nadhani ni ni wamasai walioamua kuhamia Machame, hupenda kubeba visu na pia kibiashara bado wana mwamko mdogo.

Kwa Mwarusha nae naona wanatahiri kama wamasai na kuna fimbo za bomani kama wamasai.

Waarusha na wameru ni kabila moja?

Asili yao wote ni wamasai?
We jamaa unaonekana uko deep sana kifkra, nafatiliaga nyuzi zako nyingi, huwa unaleta mada fikirishi sana, big up mkuu [emoji1307]

Sent from my SM-A235F using JamiiForums mobile app
 
Mpaka kesho siamini kama kuna kabila linaloitwa Muarusha,

Nnachofaham mimi Arusha ina makabila makuu mawili
, Masai na Chaga

Hawa wamasai ,kwa hapo arusha wamegawanyika mara mbili kuna wa mjini ambao ndo hao mnawaita waarusha na kuna wale wa ndanindani lakini wote ni wamasai

Ukija upande wa pili, hawa wanaoitwa wameru kiasili ni wachaga wa machame waliohama kutafuta maeneo miaka hiyo ndo wakaanzisha makazi yao huko meru, ila baada ya miaka kupita na muingiliano.wa jamii ya wamasai na wachaga ndo wakaform hao wameru ,na ndo maana mmeru anatabia zote mbili za kimasai na za kichaga

Kwa lugha rahisi mwenye asili ya Arusha kabisa ni Mmasai peke yake, haya makabila mengine yamekuja tuu

Kingine msichofahamu ni kwamba , Mchaga wa machame, Mmeru na Mkikuyu wa kenya wote wanasikilizana

Sent from my SM-A235F using JamiiForums mobile app
Kabila fulani kuwa na unasaba na kabila jingine siyo kitu kipya. Hakuna kabila lililoshushwa toka Mbinguni.

Kama unaamini kuwa binadamu alitokana na mwanaume na mwanamke wa kwanza kuumbwa, endapo ukifanya kufuatilia, utaishia kusema hakuna kabila.

Unafahamu asili ya Wachaga? Ni muunganiko wa makabila kadhaa: Wamasai, Wataita, Wakamba, Wasambaa, n.k. Ikiwa huamini kwamba makabila hayajashushwa toka Mbinguni bali yamejiunda hapa hapa duniani kwa kushawishiwa na mzingira yao, utasema Wachaga si kabila.

Unajua kuwa makabila mengi hapa Tanzania yanasikikizan lugha? Kama utatumia kigezo cha lugha, basi Tanzania ina makabila machache sana, labda hayafiki hata kumi.

Mengi ya makabila yaliyopo Tanzania yanasikilizana lugha.
 
Mwanamke wa kimeru sio wa kuoa atakuchinja
Nashangaa kama karne hii bado kuna watu wenye mitazamo hiyo.

Nimewaona Wameru wengi walioishi na waume zao kwa amani mpaka uzeeni, na nimeshasikia wanawake wa makabila mengine waliotuhumiwa kuhuhujumu uhai wa waume zao kwa kushirikiana na wabaya wa waume zao.

Tabia ya kuua haitokani na kabila la mtu, bali ni ushetani ambao mtu yeyote anaweza kuwa nao akiamua bila kujali kabila lake.
 
Wamasai na Waarusha ni makabila mawili tofauti japo wanasikilizana lugha.

Wameru na Wamachame wanaelewana lugha japo ni makabila tofauti.

Kimsingi, miongoni mwa makabila makuu (siyo pekee) Arusha ni Wameru, Wamasai na Waarusha.

Hayo makabila matatu yana baadhi ya desturi wanazoshea lakini kila moja lina upekee wake unaolitofautisha na jenzake.
Hakuna kabila ĺa waarusha.
Hata wao wanajiita wamasai.
 
Hakuna kabila ĺa waarusha.
Hata wao wanajiita wamasai.
Sijayachimba saana makabila ya Tanzania, lakini alau nimeyafuatilia machache kwenye vitabu na masimulizi ya wazee wakubwa. Makabila matatu ya Arusha ni miongoni mwa niliyoyafuatilia kipindi fulani kwa lengo fulani, japo niliahirisha baadaye mradi husika kabla ya kuukamilisha.

Tembelea maktaba zenye Machapisho ya Wamisionari wa mwanzoni kufika Arusha utakutana na kabila la Waarusha na jinsi walivyofika maeneo ya Arusha ya sasa.

Kulikuwa na kitabu kimoja kinachowaelezea hayo makabila matatu, nafikiri title yake ilikuwa ni WAARUSHA, WAMASAI NA WAMERU. Kilikuwa kinauzwa KIMAHAMA BOOKSHOP, ARUSHA.

Kitafute, kitakusaidia kuyaelewa usiyoyaelewa.
 
Mpaka kesho siamini kama kuna kabila linaloitwa Muarusha,

Nnachofaham mimi Arusha ina makabila makuu mawili
, Masai na Chaga

Hawa wamasai ,kwa hapo arusha wamegawanyika mara mbili kuna wa mjini ambao ndo hao mnawaita waarusha na kuna wale wa ndanindani lakini wote ni wamasai

Ukija upande wa pili, hawa wanaoitwa wameru kiasili ni wachaga wa machame waliohama kutafuta maeneo miaka hiyo ndo wakaanzisha makazi yao huko meru, ila baada ya miaka kupita na muingiliano.wa jamii ya wamasai na wachaga ndo wakaform hao wameru ,na ndo maana mmeru anatabia zote mbili za kimasai na za kichaga

Kwa lugha rahisi mwenye asili ya Arusha kabisa ni Mmasai peke yake, haya makabila mengine yamekuja tuu

Kingine msichofahamu ni kwamba , Mchaga wa machame, Mmeru na Mkikuyu wa kenya wote wanasikilizana

Sent from my SM-A235F using JamiiForums mobile app
Hapo uliposema kuwa arusha ina makabila makuu mawili masai na wachaga inatosha kuishia hapohapo kutambulika hujui unachoandika, wachaga siyo sehemu ya makabila makuu ya Arusha.
 
Mpaka kesho siamini kama kuna kabila linaloitwa Muarusha,

Nnachofaham mimi Arusha ina makabila makuu mawili
, Masai na Chaga

Hawa wamasai ,kwa hapo arusha wamegawanyika mara mbili kuna wa mjini ambao ndo hao mnawaita waarusha na kuna wale wa ndanindani lakini wote ni wamasai

Ukija upande wa pili, hawa wanaoitwa wameru kiasili ni wachaga wa machame waliohama kutafuta maeneo miaka hiyo ndo wakaanzisha makazi yao huko meru, ila baada ya miaka kupita na muingiliano.wa jamii ya wamasai na wachaga ndo wakaform hao wameru ,na ndo maana mmeru anatabia zote mbili za kimasai na za kichaga

Kwa lugha rahisi mwenye asili ya Arusha kabisa ni Mmasai peke yake, haya makabila mengine yamekuja tuu

Kingine msichofahamu ni kwamba , Mchaga wa machame, Mmeru na Mkikuyu wa kenya wote wanasikilizana

Sent from my SM-A235F using JamiiForums mobile app
chaga kwao moshi sio arusha wamehamia
 
Huna

Hujui kitu karudi Darasani toka lini mchaga akawa mojawapo ya kabila toka Arusha??
 
Waarusha ni wale wamasai wanaopatikana maeneo ya mjini.

Wameru sio waarusha ila kuna baadhi ya mila zinafanana.
 
Back
Top Bottom