matatizo yote ya maisha wanao sababisha ni wanawake!!Kwani wanawake bila ya kujalisha aliyeolewa na ambaye ajaolewa wote ndiyo wanaosababisha ugumu wa maisha
Naamini hukumaanisha ulivyosema na ni bora uwatake
radhi wanawake/wadada wote kwasababu unacho sema
si kweli.
Hii ni kama vile Adam alivyomwambia Mungu kuwa
mwanamke ndiye aliye mshawishi kula tunda. kwa
maneno mengine ni kutokuukabili ukweli (running
from the truth). Ukweli ni kwamba Adam hakuwa
na balls kusema NO to a woman.
kakakiiza ni bora kujiangalia mwenyewe unapojikwaa
kuliko kunyooshea mwingine kidole.
Mwanamke hawezi kukusababishia ugumu wa maisha
hata kidogo kwasababu binadamu tuna uwezo
wakufanya maamuzi.
katika tatizo lolote unalofikiri ni gumu kulikabili kuna
mtu aliyewahi kulikabili. Umesema mafisadi wamekamatwa
na wanawake ndiyo maana nchi ni masikini, kwani
wao ni watoto? Wao wanauwezo wa kukataa.
Kama wewe ni believer utakumbuka jinsi yusufu alivyo
mkimbia yule mama ambaye alitaka kufanyanae mapenzi
(Mwanzo 39:6-10)
Unajua unapo mnyooshea mwingine kidole inamaana
umekubali kushidwa. Yaani tatizo linakuwa kubwa kuliko
uwezo wako kwahiyo unasingizia watu wengine au
circumstances.
kama utajifunga mkanda na kumuamini Mungu huwezi
kusingizia wengine kwasababu hakuna kinachoshindikana
kwa Mungu.