Je, mpangaji huyu ana haki yoyote?

Unataka watoto wako wakaishi wapi? Hiyo tabia ya kutelekeza watoto inabidi tuipinge kwa nguvu zote.
 
Kwa mtu mwenye tabia ya umalaya anakuwa na watoto ambao wengi hawajulikani nani mzazi mwenza. Ni vizuri kuacha tabia hiyo.

Ila mimi ninachotaka kusema, kwa waafrika ni mpaka awepo mdai wa kuwa hawa watoto ni wangu au ni wako ndiyo inapalekwa kisheria na vipimo vya DNA kutumika.

Na katika mila za waafrika wengi kama mzazi wa kiume anakufa wakati hajawatambulisha watoto wa mwanamke ambaye hajafunga naye ndoa ya kimila, serikali au dini hao watoto hawatatambulika na upande wa mume. Hao watoto watakuwa kama wa beberu la jirani lililopita na kukutilia mbegu kwenye zizi lako, wanambuzi watakaozaliwa ni wako.
 
Kwahiyo Mama wa watoto hana haki ya kumtaja baba wa watoto wake mpaka aamue baba ?
 
Asubiri mume afe ndiya adai huyu alikuwa mume wangu, inaleta shida! Anatakiwa ajitokeze mume akiwa hai.
Hasemi alikuwa mumewe anasema alikuwa mzazi mwenzie,na ukiangalia watoto na baba yao kama dagaa vile(kufanana)
 
Kijamii atakuwa ana haki ya kuishi hapo, endapo atakutana na ndugu wastaarabu wenye utu.
 
Bandu Ncheche, hili ndiyo jibu sahihi, kama ndugu wakikosa ustaarabu hakai kabisa kwa mujibu wa jamii zetu.

Mama mmoja kule kijijini kwetu alifiwa na mkaza mwanae kwa ngoma enzi zile, baadaye akafiwa na mwanae yule aliyefiwa na mke.

Yule bibi alilia sana akasema kama angesikia kuwa mwanae ameringa mimba mwanamke yeyote angeenda kumkomboa, lakini haikuwa.

Sasa huyu angekuwa ndiyo huyo unayesema kusingekuwa na shida.
Kijamii atakuwa ana haki ya kuishi hapo, endapo atakutana na ndugu wastaarabu wenye utu.
 
Hakikisha mmepeana chumba kwa maandishi, mpe mkataba wa kudumu kuwa ataishi hapo milele hadi atapo jisikia yeye kwa hiari kuondoka
 
Ok nimekusoma,kwa maana hiyo Sheria haina msaada wowote ,kuendelea au kutoendelea kukaa pale kutategemeana na busara za ndugu wa marehemu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…