Je, mpira ukirushwa ukaingia golini moja kwa moja ni goli?

Je, mpira ukirushwa ukaingia golini moja kwa moja ni goli?

Scenario 4;

Timu inashambulia
1) Suarez anarusha kwenye 18 ya Madrid,hakuna aliyegusa. Mpira unaingia golini.

Maamuzi: sio goal,Goal kick. Madrid wapige

2)Suarez anarusha kwenye 18 ya Madrid. Kipa kaugusa,ukamshinda,ukaingia golini
Maamuzi:Goal. Mpira kati ya uwanja

Timu inajilinda. Mpira uko kwenye nusu yao

3)Gerrad pique anamrushia kipa wake au mwenzie aliye karibu Na goal la Barca. Mpira hajagusa MTU,unaingia golini.

Maamuzi: corner. Madrid wanakuja kupiga.

4)Gerrad Pique anarusha kwa kipa wake au MTU mwenzie wa Barca. Kipa kaugusa,ukajaa wavuni
Maamuzi. Goal. Mpira kati


Mpira wa kurushwa kuelekea golini usipoguswa ukiingia golini. Assume umetoka nje ya goli pembeni au juu. Ndio maamuzi yafuate.

Hakuna goal linafungwa kwa THROW IN bila kuguswa.

SHERIA NAMBA 15 KATIKA ZILE 17
Good

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpira wa kurushwa in fact ukishaanza kuja haujalishi origin kwenye consequences zitakazotoea kuamua impact. Hili inakuwa goli na mfungaji ni aliyerusha. Mpira wa kurushwa ni halali kwa mantiki yake. Ikiwa hivi kuwa tujali na kuheshimu taratibu za mpira basi mpira wa kichwa golini usingekuwa goli hadi iwe kwa mguu peke yake. Nawasilisha!
 
Mpira wa kurushwa in fact ukishaanza kuja haujalishi origin kwenye consequences zitakazotoea kuamua impact. Hili inakuwa goli na mfungaji ni aliyerusha. Mpira wa kurushwa ni halali kwa mantiki yake. Ikiwa hivi kuwa tujali na kuheshimu taratibu za mpira basi mpira wa kichwa golini usingekuwa goli hadi iwe kwa mguu peke yake. Nawasilisha!

Ni Vizuri kuuliza kabla ya Kuandika!

Soccer lina Sheria zake ndugu na wala haliendeshwi kwa hisia.

Mechezaji (asiyekuwa kipa kwenye Boksi lake) basi haruhusiwi kucheza mpira kwa Mkono kwa mazingira yoyote yale na ndiyo mana Mkono hauna Offside.

Mpira wa kurushwa hauruhusiwi kurushwa mchezaji akiwa ndani ya Uwanja yani kuivuuka Line/Mstari wa pembeni kwa sababu haruhusiwi kucheza mpira kwa mikono akiwa ndani ya uwanja.
Na Ndiyomana anaporusha mpira anatakiwa awe nje kidogo ya uwanja aishie kuugusa tu mstari wa pembeni.

Akisharusha mpira na ukishaingia uwanjani ndiyo unachezwa kwa miguu uwanjani.

Kwahiyo hakuna goli linalofungwa kwa mikono kama tu mpira huo haujaguswa na mtu yeyote kwa mguu au Kipa kuugusa kwa mkono kwani anaruhusiwa kucheza mpira kwa mikono kwenye eneo lake.
 
Goli mkuu, kuna mechi ilikuwa msimu wa 2003 Birmingham City na Charlton Athletic, Charlton walipata goli baada ya beki wa Birmingham kumrushia kipa mpira na akashindwa kuzuia.

Sent using Jamii Forums mobile app


Kipa alijaribu kuuzuia lakini akashindwa! Kwahiyo uliguswa kabala haujaingia Golini ndiyomana ukawa Goli
 
Gerrad pique anamrushia kipa wake au mwenzie aliye karibu Na goal la Barca. Mpira hajagusa MTU, unaingia golini.

Maamuzi: corner. Madrid wanakuja kupiga.

Hiyo Sheria Wengi hawaijui kama ipo ndiyomana Wanaishia kuwapiga Marefa kwenye Chandimu
 
Back
Top Bottom