Je, mpira una uchawi?

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Hivi uchawi unafanya kazi kwenye mpira?

Mimi nina mdogo wangu ana miaka 14 mwaka kesho hapo atakuwa na miaka 15. Sasa huyu mdogo wangu ni mchezaji wa mpira, anapenda mpira sana.

Na kwa bahati nzuri alipata bahati ya kuchukuliwa na timu ya vijana chini ya miaka 16 ya Royal Beauport. Hii ni timu kubwa tu, huku Canada inashiriki Ligi Kuu ya Canada.

Ila cha ajabu toka atue kwenye timu hii amepoteza kipaji chake, nimekuwa nikimfatilia kwa umakini amekuwa tofauti na yule wa zamani.

Kipindi cha nyuma alikuwa bora sana, kuanzia kwenye kasi, kupiga chenga, na pasi. Ila nahisi ni kwasababu kipindi cha nyuma walikuwa wanacheza tu kwenye timu za shule, kwasasa amekutana na wachezaji bora zaidi yake ndiyo maana amepotea, na akiendelea vile wanaweza kumtema kabisa.

Sasa nataka kujua je, mpira una uchawi? Labda ninaweza kufanya jambo kwa ajili yake. Napenda kuona akiendelea zaidi.
 
Uchawi kila mahali upo mpaka ibadani uki-apply unafanya yake. Ila sio kitu kizuri kwenye maisha endelevu.
Kumsaidia mdogo wetu tafuta mtaalamu (msomi) wa masuala ya mpira. Utanishukuru.
 
Wewe ndo ulijiaminisha kuwa dogo anajua mpira Ila huenda dogo hajui mpira , au kakutana na wajuvi wenzake , hakuna mchawi hapo mwambie ajiamini tuu , akomae
 
Onana na wazee wa yanga watakusaidia maana wakicheza mechi na simba wako tayari mpaka kuua ili wasifungwe hata wawe na team mbovu kiasi gani.
 
TANZANIA mpira ni uchawi nje mpira ni hesabu na timing
 
Haupo. hatuoni timu zikiroga na kufanikiwa, tunaona timu zinazonunua wachezaji wazuri na kuwekeza pesa ndizo zinafanikiwa.
 
Onana na wazee wa yanga watakusaidia maana wakicheza mechi na simba wako tayari mpaka kuua ili wasifungwe hata wawe na team mbovu kiasi gani.
Na mzee wa Unga unga wa Gadiel Michael kule Mbeya, nampataje?
 
Uchawi kila sehemu,hata ukioa muda mwingne uchawi unahitajika kumtuliza mkeo.
 
Aliyekwambia kashuka kiwango ni nan ? Unajua huko alikoenda ameambiwa acheze vp? sport academy nyingi za bongo wanafundisha watoto Mpira wa matokeo, Ila kwa wenzetu huanza kufundisha principles za mpira, katika kipindi hichi mtoto hata afungwe sio tatzo Ila afate principles alizifundishwa.
 
Mwambie avae jezi nyeusi halafu aonane na mganga wa mihogo

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
uchawi haufanyi Kazi labda Familiya yenu mmemroga ili asitoboe lakin kuroga ili awe Bora zaidi ya wenzie haiwezekani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…