Kwanza neno Bikira lina maana pana kuliko tunavyo dhania, na ubikira una pande mbili. Nadhani kuna ubikira wa kihisia na ubikira wa kimwili. Nadhani kama kweli mtu anataka asiwe bikira anatakiwa kuachana na mambo yote ya kihisia kuhusu ubikira na kujihusisha na vitendo vya ngono kimwili.
Katika tafsiri yangu hii, kitendo chochote cha ngono kinachohusisha watu kuchojoa nguo na kusisimkwa mpaka kufikia mshindo hata bila kuingiliana kimwili basi ni ngono. Nadhani kuwa uchi na kusisimuana ni ‘hatua ambayo haina kurudi nyuma', siyo kuingiliana kimwili.
Haijalishi kama kitendo hicho ni cha mwanamke na mwanamume kwa asili au ni cha wanaume kwa wanaume (mabasha na mashoga) au wanawake kwa wanawake (wasagaji), kama utashirikiana mwili wako na mtu mwingine, au kama utampa raha ya kimahaba mtu mwingine mpaka akafikia mshindo na kutoa manii au ukiwa na madhumuni atoe manii, basi umefanya ngono.
Pia nadhani kwamba ubikira siyo kitu fulani ambacho ‘unapoteza' au ‘kinachukuliwa', bali kitu fulani ambacho unashirikiana na mtu mwingine, mara moja tu katika maisha. Kama hukumpatia mtu mwingine, basi utaendelea kujihesabu kama ni bikira.
Nadhani watu ambao wamebakwa au kutomaswa bado wataendelea kuwa bikira katika hisia hata kama miili yao imefanya mapenzi. Hawajakoma kuwa bikira, na wala hawajawahi kufurahia na kuijua raha ya hisia za kimapenzi ambayo huenda sambamba na kuutoa mwili wako kwa mahaba kwa mtu mwingine.
Kama bikira yako imetolewa na mtu mwingine kwa mabavu, japokuwa ni kwa kufanya mapenzi kimwili, sidhani kama ni busara kusema kwamba wewe si bikira tena. Bado utaendelea kujichukulia kana kwamba hujawahi kufanya mapenzi, bado utaona ngono kama kitu kigeni kwako.
Kuwa mwathirika wa kubakwa hakuwezi kukakulazimu uishi na alama ambayo hukuiomba au kuitaka. Ubikira siyo kitu ambacho mtu anakipoteza kwa bahati mbaya, kutokuwa bikira ni jambo ambalo mtu analichagua mwenyewe.
Mtu aliyebakwa na kwa bahati mbaya akapata mimba, bado kwa fikra zake ataendelea kujiita bikira, na hilo linaweza lisiwe kosa kwake! Haijui raha ya mapenzi, hajui maana ya mapenzi, mpaka pale atakapoamua mwenyewe kwa nafsi yake kwamba anahitaji kufanya mapenzi, ndipo anapoweza kuamini akilini mwake kwamba si bikira tena!