Je! mtandao ukiwa na download speed kubwa ndio mzuri ?

Je! mtandao ukiwa na download speed kubwa ndio mzuri ?

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Posts
31,559
Reaction score
42,179
Watu wengi wanalalamika speed ya kubrowse ni ndogo, hawezi kuangalia video online, wengine wakipiga viber japo speed kubwa lakini hawasikilizani, kuna wengine video chat na hata wacheza magame online wanalalamika. Vitu vyote hivi tunamsingizia download speed je ni sahihi? Mtandao ukiwa na speed kubwa ya kudownload basi vitu vyote hivi vitakuwa sawa?

Jibu ni hapana unaweza kuwa na speed kubwa ya kudownload hata 5gb per second lakini usiweze kuongea viber wala kuchat video skype sababu si download speed inayo determine mambo mengi bali ni latency na ping ndio wabaya wetu hasa hapa Tanzania.

Ni nini latency na ping?

Latency- huu ni muda ambao unachukua kuomba kitu kutoka server.(one way trip)
Ping-huu ni muda ambao unaomba kitu kutoka server hadi server kukujibu wewe (two trip)

Hivyo hapa chini nitaongelea zaidi kuhusu ping na jinsi inavyokuathiri.

-SI unit ya ping ni millisecond na ikumbukwe millisecond 1000 ni sawa na 1 second(sekunde)

Hivyo tunaona hapa kumbe kuna muda hupotea kuomba kitu kwenye server hadi kujibiwa, mfano nataka kuingia JamiiForums nikiandika jamiiforums then nikabonyeza enter kuna muda utapotea kabla sijaanza kupokea data za Jamiiforums kwenye browser yangu. Huu muda hutofautiana kutokana na mtandao/isp unayotumia. Hebu tuangalie hizi screenshot mbili

7918764_f520.jpg

Speedtest-Chicago-Ping.png


Screenshot ya kwanza jamaa ana download speed 8.41mb/ps na ping ya 700ms
Screenshot ya pili jamaa ana download speed 1.5mb/ps na ping ya 34ms

Hivyo kikawaida utasema jamaa wa kwanza mkali sababu speed yake kubwa lakini unasahu inamchukua sekunde 0.7 kusubiri kila anapoclick, jamaa wa pili speed yake sio kubwa sana ila inamchukua sekunde 0.03 tu kusubiri hivyo kwenye viber, kubrowse, video chat na video game jamaa wa pili anampita wa kwanza kirahisi kabisa.

Maeneo gani ukiwa na download speed kubwa unapeta?
1.Unapodownload kitu chochote iwe video/torrent/audio/picha/whatsap nk
2.Unapoangalia video online zenye buffer kama youtube

Maeneo gani ping ikiwa faster unapeta?
1.Ukiongea kwa sauti (viber) au kwa video (skype) online
2.Ukiwa unabrowse
3.Ukicheza games online
4.Ukiwa unaangalia video online lakini zinaupdate in realtime mfano kuangalia mpira wa miguu live.

Hivyo tukichagua mtandao tusiangalie tu speed ya kudownload bali hata ping

Upload speed
Upload speed nayo ni muhimu pia hasa kwa webmaster na wanaochat na kupiga simu online. Unapoongea na mtu na viber inabidi kile ulichoongea kitumwe kwenye server kabla hakijamfikia uliempigia hivyo kunahitaji uwe na upload speed nzuri ili kifike haraka na kwa webmaster/youtubers nk nao wanahitaji upload speed nzuri ili kueka vitu vyao youtube au kwenye website zao.

Ningeomba kama kuna mtu anatumia ethernet ya TTCL au kampuni nyengine za internet watuekee screenshot za ping zao ili tulinganishe na hii mitandao yetu ya kina tigo na airtel tuone tunamiss nini.
 
Umetoa taarifa nzuri sana Chief.
Salute to you.
Kwann wizara ya mawasiliano haifanyi mchakato wa kuboresha mambo haya na kuwa strong-arm makampuni ya isp kuwa katika standards.
Kuna wakati nilisoma report moja online baada ya kuwa nmesikitishwa sana na uwezo wa internet hapa nchini kwetu na bei zake pia. Kwenye report hii ambayo iliandikwa na watu wanaoprovide bandwidth kwa mkonge wa taifa walisema kuwa wanaiuzia nchi yetu kwa bei rahisi sana na uwezo ni wa juu lakini wanachoshangaa ni kuwa customers wanakuwa charged bei kubwa kwa uwezo mdogo. Hadi wakaendelea na kusema kama tunahitaji tupunguziwe bei tuseme ili watu wengi zaidi wa uwezo wa juu na chini wawe na easy access ya information .
Tazama tunavokuwa tunaendelea kuaibika kila kukicha.
 
Last edited by a moderator:
Umetoa taarifa nzuri sana Chief.
Salute to you.
Kwann wizara ya mawasiliano haifanyi mchakato wa kuboresha mambo haya na kuwa strong-arm makampuni ya isp kuwa katika standards.
Kuna wakati nilisoma report moja online baada ya kuwa nmesikitishwa sana na uwezo wa internet hapa nchini kwetu na bei zake pia. Kwenye report hii ambayo iliandikwa na watu wanaoprovide bandwidth kwa mkonge wa taifa walisema kuwa wanaiuzia nchi yetu kwa bei rahisi sana na uwezo ni wa juu lakini wanachoshangaa ni kuwa customers wanakuwa charged bei kubwa kwa uwezo mdogo. Hadi wakaendelea na kusema kama tunahitaji tupunguziwe bei tuseme ili watu wengi zaidi wa uwezo wa juu na chini wawe na easy access ya information .
Tazama tunavokuwa tunaendelea kuaibika kila kukicha.

tanzania content tunapewa ya kutosha zipo bundle hadi za 15,000 unapewa unlimited data, tatizo ni speed. maeneo mengi unakuta hadi saa 8 usiku ndo unapata speed ya kueleweka mchana kitu kinakuwa kobe tu.
 
Last edited by a moderator:
Post nimeikubali chief ila swali langu kwako moja tu, profile yako imeandikwa Likes given:0, hamna post hata moja humu JF ambayo ushawahi kukaa ukaikubali?

Ha ha ha we jamaa umenifurahisha afu uwa mnanichanganya Dreson4 na Dreson3
chief mkwawa said:
ni nini latency na ping?
latency- huu ni muda ambao unachukua kuomba kitu kutoka server.(one way trip)
ping-huu ni muda ambao unaomba kitu kutoka server hadi server kukujibu wewe (two trip)
hivyo hapa chini nitaongelea zaidi kuhusu ping na jinsi inavyokuathiri.
-SI unit ya ping ni millisecond na ikumbukwe millisecond 1000 ni sawa na 1 second(sekunde)
hivyo tunaona hapa kumbe kuna muda hupotea kuomba kitu kwenye server hadi kujibiwa, mfano nataka kuingia jamiiforums nikiandika jamiiforums then nikabonyeza enter kuna muda utapotea kabla sijaanza kupokea data za jamiiforums kwenye browser yangu. huu muda hutofautiana kutokana na mtandao/isp unaetumia
Somo zuri sana!
 
Last edited by a moderator:
tanzania content tunapewa ya kutosha zipo bundle hadi za 15,000 unapewa unlimited data, tatizo ni speed.maeneo mengi unakuta hadi saa 8 usiku ndo unapata speed ya kueleweka mchana kitu kinakuwa kobe tu.
Kwa hiyo hili swala linasababishwa na nini hasa.

Je lipo ndani ya uwezo wa mitandao yetu. Au TCRA.?

Nini kinaweza kufanyika kukawa na speed ya kutosha kwenye net.
 
Back
Top Bottom