Je! mtandao ukiwa na download speed kubwa ndio mzuri ?

Kwa hiyo hili swala linasababishwa na nini hasa.

Je lipo ndani ya uwezo wa mitandao yetu. Au TCRA.?

Nini kinaweza kufanyika kukawa na speed ya kutosha kwenye net.

uwezo wa mitandao na msongamano wa watu unachangia kiasi kikubwa. mimi huku nilipo napata speed kubwa sana ya internet sababu watumiaji ni wachache, ila sehemu zenye misongamano speed huwa mbaya sana sababu mitandao yetu hutoa shared speed. na waki upgrade vifaa vyao ili kuweza ku acomodate watu wote hawa bila speed kushukua basi ujue hata bei watapandisha maana ni gharama kubwa.

sjui wana mpango gani na huu mkonga ila ningependa kuona makampuni yanasambaza internet za cable/wifi majumbani ili tupunguze kutegemea hizi mobile data. ttcl wana huduma hii lakini nafikiri bado hawajakuwa serious ili ku compete na mobile data. kwa nchi za wenzetu sasa hivi broadband plan zao zinarange dola 40-60 kwa speed ya 100mbps ambayo ni kubwa sana. kwa sababu hapa bongo watu wanapenda virahisi tunahitaji angalau kampuni ambayo itaweza kutoa internet ya 8-20mbps kwa 20,000 hadi 50,000 kwa mwezi.
 

Shukrani mkuu kwa jibu zuri.

Hivi hii huduma ya WiFi speed yake inakuaje.
Yaani ubora wake nini ukitofautisha na data.
 
Shukrani mkuu kwa jibu zuri.

Hivi hii huduma ya WiFi speed yake inakuaje.
Yaani ubora wake nini ukitofautisha na data.

hata kwa mobile data unaweza tengeneza wifi, point yangu kubwa ni kwamba hawa watu watumie mkonga/fibre kusambaza internet kwa waya au wifi. hivyo ina maana wifi itategemeana na speed ya mkonga.

uzuri wa wifi ni kwamba ina capacity kubwa mfano 3g mwisho wa speed ni 42mbps wakati wifi zipo hadi za 1gbps.

watu wakisambaziwa internet hizi zenye speed mobile data zitabakia zitumike kwenye simu na maeneo mengine ambayo wana matumizi madogo.
 
hapa natumia proxy na tigo zina latency mbovu sana nisingependa nizitumie hapa sababu zitaonesha ping kubwa. ila muda sio mrefu nitaeka za airtel utaizona

Nasubiri za airtel mkuu maana mimi nawaminia airtel teena saana
 
Kaka tujuane maana naona hubaatishi kwenye haya mambo kama IT wetu wengine vmeo saana. Lakini CHIEF-MKWAWA basi uwe unajaribu kutoa like kwa wenzio mbona sisi tunakupa kwa kazi yako nzuri unayotufanyia.
 
I tested with Airtel leo on laptop na simu, and I must say I'm blown away with the speed. I've been using it for video calls and watching videos online in HD and ime-perform vizuri but I never cared kutest speed! But today I salute them because my experience with them zamani was horrible.


Almost similar performance on laptop na simu but ping is way off. NB: I tether my phone connection to my laptop
 
mbona kwenye iphone ping ni ndogo? au kulikuwa na background task zinatumia data

No idea why, but I usually have minimal tasks running in the background. I'll give another shot when I disconnect it from the laptop.
 

Kweli kabisa mkuu.
Unachosema naafiki kabisa.
 
Nifanyeje ili niweze kuona izo speed za download na upload na ping kwenye smartphone?
 
Kaka mwisho wa siku ni speed tu. Hiyo ping inaweza kuwa kubwa au ndogo kutegemea na bottlenecks kwenye intermediate nodes au labda uplink kutoka kwa ISP kwenda kwa global ISP. Na bottlenecks nyingine huwa zinasababishwa na slow processing routers and gateways. Ila mwisho wa siku hiyo round trip ya ping inategemea na speed ya route nzima iliyotumika kutuma request. Ukiwa na 5 mbps down link halafu somewhere in between kuna router ambayo maximum processing capacity yake ni 1 mbps lazima usubiri.

Nachojaribu kusema ni kuwa ping round trip na latency ni vitu vinavyotegemea speed ya route nzima sio tu ile iliyopo kati ya mtumiaji na ISP.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…