Bw.Dotori pamoja na Wadau wote naomba nianze kwa Kuomba Samahani,na Msamaha huu ni kuwa ntatoka nje ya Mada hii Kidogo.
Tumekuwa hadi hii Leo na Viongozi(Watawala) tulowachagua ktk Awamu nne tofauti(Zingatia Kung'atuka kwa Mwalimu)ndani ya misingi 'safi kabisa ya Kidemokrasia',na dhamira Kuu ya Watanzania wote kwa kuwachagua Watawala hawa ni ili basi watujengee Mazingira na Misingi bora Tujikwamue katika Dimbwi la Umasikini wa: Hali, Kiakili, Mali.
Tofauti yake ni kwamba:
Dimbwi hili la Umasikini limekuwa likiongezeka KINA kila Awamu,na watanzania walio Vijijini na hata Mijini, wazidi Kuzama kwasababu ya Afya Duni,Ujinga na Ulofa ulokidhiri,matokeo yake
Watanzania tunaishi Kimiujizaujiza tu,hakuna mipangilio,bora Liende!kwa mfano:Upo ndani ya daladala, kwa wale tunaoishi kati ya maeneo ya Magomeni(Mapp) na Fire, kila siku ya Mungu Unaona Kundi la watu,hawana vikapu mikononi,mabegi,au hata Ndoo za maji basi, likiwa kwa miguu linakatiza maeneo ya jangwani linaelekea katikati ya Jiji,watu wanajikusanya na kukaa katika vikundi ili kupiga Gumzo tu(Vijiweni)kwa kweli Nnajiuliza Maswali mengi sana pasipo majibu!!
Kuna usemi kuwa Muda kamwe Hauongopi!
Labda ni Uzee Unaingia au napatwa Na Wendawazimu sijui!,lakini yapata Miaka 40 hivi, kwa kweli sijaona Umuhimu/Sababu ya KUWA NA RAIS NCHINI TANZANIA.Nnaelekea kufikiri basi hata tukaweka PAKA MWITU pale Ikulu,bado hilo li-Nchi litakwenda tu!!